Mbunge Aliyeitosa CHADEMA na Kuhamia CCM Apangua Tuhuma za Kuandikiwa Barua

Aliyekuwa Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul amejibu madai ya baadhi ya makada wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA wanaomshutumu kuandikiwa barua ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kutokana na barua hiyo kuwa na kasoro na kufanana na barua zingine za wabunge waliojiuzulu kabla yake.

Gekul amesema kuwa wanadamu wakiamua kukutaftia kosa hawawezi kukosa cha kuongea hivyo amewataka Chadema wahangaike kujibu hoja zake na si kuanza kuangalia vitu binafsi.

“Wanadamu wakiamua kutafuta makosa kwako hawayakosi, utakuwa mtu wa ajabu unayeangalia zaidi maandishi badala ya ujumbe wa barua, uandishi wa barua mimi siangalii, kwangu sikuona kama ni hoja.”amesema Gekul

Amesema kuwa makosa ya kiuandishi hutokea popote, hivyo kukosewa kuandikwa kwa barua yake ya kujiuzulu sio tatizo lakini chamsingi ni ujumbe umefika sehemu husika na wala sio lugha iliyotumika, hivyo amewataka wahangaike na kujibu hoja zake.

Hivi karibuni katika mtandao wa Twitter afisa habari wa CHADEMA, Tumaini Makene alikosoa uandishi wa barua za wabunge waliojiuzulu kwa madai kuwa ni za aina moja.

Pauline Gekul ametimiza idadi ya wabunge 8 kutoka vyama vya upinzani waliotangaza kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai mbalimbali ikiwemo kumuunga mkono Rais Magufuli.


from MPEKUZI

Comments