Masaa 24 Yamepita Mo Dewji Bado Hajapatikana...Watu 12 Wamekamatwa Kusaidia Polisi

Ni masaa 24 toka bilionea kijana Mo Dewji atekwe na watu wasiojulikana jana Alhamisi akiwa GMY ya hotel ya Colosseum Oysterbay jijini Dar es salaam na mpaka muda huu hakuna taarifa mpya.

Taarifa ya mwisho jana kutoka kwa Kamanda wa Polisi kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ilisema watu wanaoshikiliwa kwaajili ya mahojiano kutokana na tukiohilo ni 12.

Mambosasa alisema kuwa watu hao wanashikiliwa  ili kusaidia uchunguzi wa tukio hilo , kati ya hao waliokamatwa ni pamoja na walinzi wa hoteli ya Collesium, mahali ambapo tukio hilo lilitokea.

Akizungumza jana na Clouds Fm, dereva wa Mo Dewji  alisema kuwa lilikuwa ni jambo la kawaida kwa mfanyabiashara huyo tajiri kuendesha gari lake mwenyewe kwani alikuwa anaamini ana amani.

“Mo Dewji ni tajiri lakini anaishi maisha fulani hivi kama vile sio tajiri. Yaani alikuwa hana hofu na raia kwa sababu yeye kila mtu anayekutana naye ni kama vile anajuana naye miaka mingi,” alisema.

Dereva huyo ambaye amefanya kazi kwa Mo tangu mwaka 2001 ameeleza kuwa Mo alikuwa anajiamini na hakuwa na uoga dhidi ya raia, lakini aliwahi kumtahadharisha mwaka huu kuwa amekuwa akipokea jumbe za vitisho.


from MPEKUZI

Comments