Madereva wa wa Mabasi mwendokasi Dar wakimbia na funguo

Kampuni inayotoa huduma ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es salaam (UDART) hatimaye imetoa ufafanuzi kuhusiana na vurugu zilizotokea leo katika kituo cha mabasi hayo cha Kimara jijini Dar es salaam, baada ya kukosekana kwa usafiri huo kwa takribani masaa 3.

Msemaji wa UDART Bw. Deus Bugaywa amesema chanzo cha tukio hilo ni hujuma zilizofanywa na baadhi ya madereva mishale ya saa 9 alfajiri, baada ya kuziba lango kuu la kutokea magari upande wa mbele pamoja ya hali kadharika wa nyuma kwa kuegesha mabasi yenye urefu wa mita18 na kusababisha usumbufu uliojitokeza.

"Baada ya mabasi matano ya kwanza kutoka ndani dereva mmoja alichukua basi na lenye urefu wa mita 18 9articulated bus na kuliegesha eneo la ndani ya lango kuu la kutokea upande wa mbele hivyo kuziba njia na wakati huo huo dereva mwengine aliziba lango la mbele la nyuma kwa basi lenye ukubwa huo huo."amesema Bw. Bugaywa.

"Baada ya kufanya tukio hilo madereva hao walikimbia na funguo za mabasi hayo kusikojulikana na walinzi walijaribu kuwafatilia lakini hawakufanikiwa kuwapata" ameongeza.

Aidha Bw. Bugaywa ameomba radhi wananchi kwa usumbufu uliojitokeza kituoni hapo huku akikanusha taarifa za ucheleweshaji wa mishahara ya wafanyakazi hao kutohusishwa na tatizo hilo.

"Tunapenda kufafanua kuwa mishahara ya wafanyakazi ya mwezi Septemba imeanza kulipwa tokea Oktoba 9, 2018 na hatuoni sababu ya kuunganisha suala hilo na mishahara; tayari tumepeleka suala hilo mbele ya Jeshi la polisi na hatua za kiuchunguzi zinaendelea ili kuwabaini waliofanya uhalifu huo"


from MPEKUZI

Comments