Lori la Oil Com lakutwa na pombe kali na Vipodozi Vilivyopigwa Marufuku

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya, linalishikilia lori la mafuta mali ya Kampuni ya Oil Com, baada ya kukutwa limebeba vipodozi na pombe  vilivyopigwa marufuku kuingia nchini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, amesema gari hilo lenye namba za usajili T 233 CXL limekamatwa eneo la Mbarali jijini hapa, jana saa nane mchana, likitokea nchini Zambia.

Kamanda Matei amesema katoni 15 za vipodozi na katoni mbili za pombe kali zimekutwa ndani ya gari hilo.

Amesema dereva wa gari hilo anatafutwa na polisi kwani baada ya gari hilo kukamatwa alifanikiwa kukimbia.


from MPEKUZI

Comments