Kumbukumbu Ya Miaka 19 Ya Kifo Cha Hayati Baba Wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

KUMBUKUMBU YA  MIAKA 19  YA KIFO CHA HAYATI BABA WA TAIFA MWL. JULIUS KAMBARAGE  NYERERE.

✍🏻Taifa letu Tanzania leo tunamkumbuka Shujaa wetu na Kiongozi wetu Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere. Mwl. Julius Nyerere alikuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania ambaye alizaliwa Mwaka 1922 na baada ya Kulitumikia Taifa lake alitwaliwa na Mwenyezi Mungu tar. Oktoba 14, 1999 Huko Uingereza Katika Hospitali ya St. Thomas. Ameishi Miaka Takribani 77.

✍🏻Tunamkumbuka Baba wa Taifa kwa Mengi aliyoifanyia Nchi yake na Taifa lake Tanzania. Amekuwa Kiongozi Mzalendo wa Kweli Katika Taifa lake, Mchapa Kazi.

✍🏻 Baba wa Taifa aliacha Kazi yake ya Ualimu na Kuchagua Siasa kama njia Sahihi ya Kulikomboa Taifa lake Tanganyika. Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere aliongoza Mapambano dhidi ya Wakoloni ili Kudai Uhuru Wetu. Wakati wote alikuwa ni Adui wa Rushwa, Maradhi, Ujinga, Ufisadi na mambo Mengine mengi aliyoamini ni Adui wa Maendeleo ya Taifa letu.
✍🏻Ijapokuwa Tuna Makabila Mengi Tanzania, Baba wa Taifa alifanikiwa Kuwaunganisha Watanganyika na kuwafanya kuwa wamoja na kuishi kwa Upendo na Kuongea Lugha Moja.

✍🏻Leo tunapoadhimisha hii Siku Muhimu ya Kumkumbuka Hayati Baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere, ni vyema tukakumbuka Mambo Muhimu ambayo Baba wa Taifa aliyakataa na kuona ni Mambo ambayo yanaweza Kutugawa Watanzania; Tukatae Kubaguana Kwa Udini, Ukabila, Kutoheshimu Utu wa Watu. Isitokee Mtu ama Kiongozi yeyote akatubagua kwa Nyanja hizo huyo atakuwa ni Adui namba moja wa Taifa letu. Mwl. Nyerere alikuwa Kiongozi nambari Moja Kulinda Rasilimali za Taifa letu ambazo ni Urithi Kwetu na Vizazi Vyetu Vijavyo.  Mwl. Nyerere Baba wa Taifa alihimiza Watu Wafanye Kazi kwa Bidii ili Kujikomboa na Umasikini lakini pia Kufanya Kazi kwa Bidii ni Chachu ya Maendeleo ya Taifa letu.

✍🏻Nichukue nafasi tena kuwaomba Watanzania Wote kuungana  na Mzalendo Mwingine Nambari Moja wa Taifa letu Mwl. Dkt .  John Pombe Magufuli, Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Kufanya Kazi kwa Bidii Kama ambavyo husisitiza Mara kwa Mara Kwamba Serikali yake  Ifanye Kazi kwelikweli na WanaNchi tufanye Kazi kwelikweli na Kwa Bidii, Kulinda Raslimali za Nchi yetu kama ambavyo alionyesha Kupitia Sakata la Makinikia, Kuendeleza Mapambano dhidi Rushwa, Maradhi, Umasikini, Ufisadi, Udini, Ukabila na Kwamba Juhudi hizi za Rais wetu Mpendwa John Pombe Magufuli ni za Kuungwa Mkono na Watanzania Wote wenye Mapenzi Mema na Taifa letu huku Tukitambua Hakuna Mtu wa nje  atakayekuja Kutujengea Nchi yetu isipokuwa ni Sisi Watanzania wenyewe ndiyo tutakaoweza kusimama imara na Kuijenga Tanzania tunayoitaka.

✍🏻Nimalizie kwa Kumpongeza sana Rais Wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli Kwa Kuchapa Kazi na Kutuletea Maendeleo Watanzania.  Ni hakika ya Kwamba anatembea ndani ya dira ya Hayati Baba wa Taifa Mwl. J.K Nyerere na Dira &  Muelekeo wa Serikali yake atakayoiunda kuwatumikia Watanzania  aliyoitoa Mwaka 2015 wakati wa Ufunguzi wa Bunge baada ya Kuapishwa kuwa Rais wa Hawamu ya Tano.

✍🏻MUNGU Ibariki Tanganyika, MUNGU Ibariki Zanzibar, MUNGU Ibariki Tanzania na MUNGU mmbariki Rais wetu Mpendwa Mwl. John Pombe Magufuli pamoja na Viongozi wengine Chini yake akiwemo Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali  Mohammed Shein.

Robert PJN Kaseko
Mjumbe Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Arusha.
Oktoba 14, 2018


from MPEKUZI

Comments