Engineer wa TANESCO afikishwa Mahakamani

Mhandisi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Stanslaus Simbila amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kutumia madaraka yake vibaya ambayo yamepelekea Kampuni ya Zwart kupata kiasi cha EURO 491,622.42 sawa na BILIONI 1,293,248,789.

Akisomewa kosa lake na Wakili wa Serikali, Iman Nitume mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wanjah Hamza amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja.

Inadaiwa kuwa kosa hilo ni kutumia madaraka yake vibaya, ambapo amelitenda kati ya June 9 na 19,2010.

Anadaiwa akiwa kama Mhandisi wa TANESCO na Meneja mradi PA/001/08/HQ/G/123 kati ya TANESCO na Kampuni ya Zwart Technick B.V kwa nia ovu alisaini cheti kilichopelekea kampuni hiyo kupata EURO 491,622.42 kabla ya kumaliza kazi waliyopewa.

Baada ya kuelezwa hayo, mshtakiwa alikana kosa hilo ambapo Wakili Nitume amedai kuwa upelelezi upo katika hatua ya mwisho kukamilika.

Mshtakiwa aliachiwa kwa dhamana ya wadhamini 2, waliowasilisha hati ya Mali ya Sh.MIL 100. Kesi imeahirishwa hadi November 8,2018.


from MPEKUZI

Comments