Dreamliner Yashindwa Kuipeleka Taifa Stars Cape Verde.....Serikali Yakodi Ndege Nyingine

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars usiku wa leo October 9 2018 itasafiri kuelekea Cape Verde kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika AFCON 2019 nchini Cameroon, Taifa Stars awali walikuwa wasafiri na ndege ya Air Tanzania Dreamliner lakini imeshindikana.

Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Dr Harrison Mwakyembe amethibitisha kuwa  Dreamliner haiwezi kwenda na badala yake wamekodi ndege nyingine maalum kwa ajili ya safari hiyo, Dreamliner imeshindwa kwenda kutokana na uwanja wa ndege waliopaswa kutua haiwezi kupokea ndege kubwa kama Dreamliner.

“Tumemtuma Mgohi aweze kuangalia namna sehemu ilivyo tutakayofikia, ametuambia kwamba uwanja ni mdogo kwahiyo tumeongea na wenzetu wa Airt Tanzania na tumeagiza ndege nyingine ambayo ina usajili wa Tanzania ambayo ina weza kushuka na kupaa kiurahisi,” alisema.


from MPEKUZI

Comments