Avril Ampa mkono Khaligraph Jones kwa kupeperusha Bendera ya Kenya Marekani

Staa wa muziki na Muigizaji kutoka nchini Kenya, Judith Nyambura Mwangi a.k.a Avril amempa pongezi ya ushindi wa tuzo ya AFRIMMA 2018 rapa Khaligraph Jones.

Mrembo Avril alimpongeza Khagraph kwa tuzo ya ushindi ya kipengele cha ‘Best Rap Act’ cha tuzo zilizofanyika usiku wa kuamkia jana  huko Dallas Texas Marekani.

Avril alindika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Instagram ulioambatana na Picha ya Khaligraph Jones.

“Waking up to great news .. congratulations @khaligraph_jones 🙌🏼 #BestRapAct 🇰🇪 #Afrimma 🇰🇪 #KenyaToTheWorld #KeepYourOwnPace ”

Khaligraph Jones aliwapiga chini wakali wenzake kibao kwenye kipengele hicho cha tuzo .Pia Khaligraph alipata nafasi ya kutoa burudani kwenye jukwaa la Tuzo hizo zilizowakutanisha mastaa mbalimbali kutoka Afrika.


from MPEKUZI

Comments