Alikiba, Diamond, Harmonize, Vanessa Mdee Waambulia Patupu AFRIMMA 2018

Usiku wa kuamkia jana kulitolewa tuzo za African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) 2018 nchini Marekani.

Wasanii wote kutoka Tanzania waliotangazwa kuwania tuzo hizo wametoka mikono mitupu, huku wasanii kutoka Kenya na Uganda wakifanya vizuri.

Wasanii wa Bongo wa Fleva waliokuwa wakiwania ni pamoja na Jux, Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz, Navy Kenzo, Alikiba, Harmonize, Vanessa Mdee na Nandy.

Rapper kutokea nchini Kenya, Khaligraph Jones ameshinda kwenye kipengele cha Best Rap Act, huku Eddy Kenzo kutoka Uganda kwenye kingele cha The East African Artist of the Year.


from MPEKUZI

Comments