Alichosema Lulu Diva kuhusu muziki wa Hamisa Mobetto

Muimbaji Lulu Diva amesema Mwanamitindo Hamisa Mobetto ni mtu ambaye amekuwa akimvutia zaidi kutokana na kazi zake za kila siku na hasa alipoingia kwenye muziki.

Kwenye Mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema licha ya Hamisa kuwa mwanamke mrembo na maarufu bado anajitahidi kufanya kazi zake na sio kutegemea kupewa tu.

"Hamisa ananivutia anapokuwa anajituma,  msichana ambaye anapigana kwa kile ambacho anakihitaji, unajua wasichana wengi wanafikiri ukishakuwa mzuri basi unaweza ukapata chochote kwa kutumia uzuri lakini mimi naona kwa Hamisa ni tofauti kidogo pamoja ni mama wa watoto wawili, kwa hiyo naona anajitihadi," amesema Lulu Diva.

Licha ya Hamisa kuwa Mwanamitindo kwa sasa ameingia kwenye muziki ambapo ameachia wimbo wake wa kwanza uitwao Madam Hero, huku Lulu Diva akifanya vizuri na wimbo  wake mpya unaokwenda kwa jina la Alewa ambao amemshirikisha Producer S2kizzy.


from MPEKUZI

Comments