AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 97 na 98 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
Huyo dada ambaye ananieleza huyu dereva bodaboda, hafananii kabisa na Linda, kwa maana Linda ni mweusi japo ni mrefu kiasi.
“Alitoka katika mazingira ya aina gani?”   
“Alitoka anakimbia, tena kama picha nilimpiga kwenye simu yangu, yaani ni bonge la totozi”
Dereva bodaboda alizungumza huku akinipatia simu yake, nikaichukua na kuitazama picha hiyo. Sikuamini macho yangu baada ya kumuona Yudia kwenye hii picha akiingia kwenye gari la Linda, jambo  lililo nifanya nijikute nikianza kufura kwa hasira kwa maanaYudia na mwenzake na K2 bado wananiandama sana kwenye maisha yangu.

ENDELEA       
Nikiwa katika hali ya mshangao, nikaona kitanda cha wagojwa, kikiingizwa kwenye gari la wagojwa, kwa haraka nikakimbia hadi kwenye gari, madaktari wakajaribu kunizuia ila nikawazidi nguvu kwa maana nimemuona Linda akiwa yupo hoi maututi.
 
“Ni mke wangu”   
Nilizungumza huku machozi yakinilenga lenga, daktari alipo niona ninamaanisha kwa kile ninacho kizungumza akaniruhusu  ili niweze kumuona Linda, ambaye niliweza kumfahamu mkono wake alio  vaa saa, ambao  ulikuwa unaning’inia kwenye kitanda.
“Linda, Linda”   
Nilimuita huku nikiwa ninamtazama uso wake ambao umechakaa kwa kuungua kwa moto na mwili wake una majeraha mengi ya moto.
“Da….dy Dany”
Linda aliniita kwa sauti ya chini sana iliyo zidi kunitisha.
“Ndio nipo hapa nipo hapa mpenzi wangu”
“Ch….chuk….”
Linda alizungumza maneno huku akifumbua kiganja cha mkono wake wa kulio japo umeungua sana, ila akajikaza sana. Nikaona kadi ndogo ya kuhifadhia kumbukumbu, nikaichukua taratibu huku nikiendelea kumtazama usoni mwake.
 
“N….ili…pi…zie kisasi”
Linda aliendelea kuzungumza kwa sauti ya kukata kata huku hali yake ikiwa mbaya
“Kaka tunakuomba utoke tumuhudumie mgonjwa”
“Dany…..ni…ni…nakupendaa……”
Linda baada ya kuzungumza maeneno hayo akatulia tuli, kwa haraka madaktari wawili wakaanza kuhangaika naye huku wakinihitaji niweze kusogea pembeni kwa maana gari lilisha anza kutembea. 

Machozi yakaendelea kunimwagika usoni mwangu, sikuamini kwamba Linda anakufa kirahisi namna hii, ikiwa ni msichana ambaye alikuwa na malengo makubwa sana kwenye maisha yake. Kila madaktari walivyo jitahidi kuhakikisha kwamba wanajaribu kuyaokoa maisha ya Linda wakawa wamechelewa, hadi tunafika hospitali ya Bombo, Linda, akashushwa kwenye gari, akapakizwa kwenye kitanda ambacho hakupelekwa tena kwenye wodi ya kuhudumiwa, ila moja kwa moja akapelekwa kwenye jengo la kuhifadhia maiti jambo lililo zidi kuumiza moyo wangu.
“Dokta nitahitaji maiti yangu kuifadhiwa hadi niweze kurudi”
“Hapa maiti ikikaa kwa muda mrefu huwa manispaa inachukua jukumu la kumzika”
 
“Hata kama, ila hakikisha kwamba maiti yangu inakaa kwa kipindi chote hadi pale nitakapo rejea, akizikwa kabla  ya mimi kurudi, basi utachukua nafasi yake”
Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na hasira sana, hadi daktari akabaki akiwa amenitumbulia macho nikatazama namba ya droo ambayoa ameingizwa Linda, nilipo hakikisha nimeihifadhi vizuri kichwani mwangu nikatoka katika jengo hili la kuhifadhia maiti, huku kichwa changu kikiwa kinamfikiria ni kitu gani ambacho ninaweza kumfanya Yudaia ambaye tayari alisha futika kwenye kichwa changu, ila kwa hili nitahakikisha kwamba nilazima ninamuua tena kwa mateso ambayo hajawahi kuyafikiria kwenye maisha yake kwamba yatatokea kwenye maisha yake.
 
Kitendo cha kutoka nje ya geti la hospitali, nikakumbuka namba niliyo pewa na binti wa kiarabu kwenye duka la kubadilishia pesa, nikakitoa kikaratasi kwenye mfuko wangu nikaitazama namba ya simu ambayo ameiandika. Nikatazama huku na kule, kwenye mabenchi ya kusubiria wagonjwa, nikawaona baadhi ya vijana wakiwa wamekaa wakichezea chezea simu zao. Nikapiga hatua hadi walipo.
“Madogo niaje?”
“Poa poa bro”
“Oya dogo simu yako ina vocha hapo, kuna mtu nahitaji kumpigia”
“Yaaa ina bando la kutosha”
“Ninakuomba uniazime”
“Poa ila pigia hapa hapa si unajua mjini hapa”
“Usijali dogo”
Dogo akanipatia simu yake, nikaanza kuingiza namba ya simu ya binti wa kiarabu. Kwa bahati nzuri namba yake ikaanza kuita, haikuchukua hata sekunde nyingi ikapokelewa.
“Mambo vipi?”
“Safi nani?
“Dany, ni muda mchache nilitoka hapo dukani kwako, nilikuja kubadili pesa za kikenya”
“Ahaa Dany mambo vipi, upo wapi?”
“Nipo Bombo hapa hospitalini, kuna mgonjwa nilikuja kumuona”
 
“Sawa, ninaweza kuja kukuchukua?”
“Ndio maana nikakupigia, ila namba sio ya kwangu, mimi nimekaa kwenye hizi benchi ukija hapa utanikuta nimekaa”
“Sawa nipe dakika kumi na tano nitakuwa nimesha fika hapo”
“Sawa”
Nikakata simu, nikamkabidhi dogo simu  yake huku nikimpatia noti ya shilingi elfu kumi kama asante.
“Asante sana kaka”
“Usijali dogo”
Nikakaa benchi hizi huku nikiendelea kufikiria ni wapi ambapo ninaweza kumpata Yudia. Nikatazama memory card hii ambayo nimepatiwa na Linda. Sifahamu ndani imehifadhiwa vitu gani ila nina hamu sana ya kuweza kufahamu ni kitu gani ambacho kipo humu ndani. Gari nyeusi iana ya Toyota Harrier ikasimama pembeni ya benchi hizi, honi ya gari hilo likamfanya kila mtu aliye kaa katika hii sehemu kulitazama gari hili, kioo kikashushwa nikamuona binti wa kiarabu akiniita, nikanyanyuka na kumfwata sehemu alipo.
 
“Ingia”
Alizungumza, nikafungua mlango wa mbele wa gari, nikaingia nikatzama siti ya nyuma hakuna mtu. Binti huyu akafunga kioo cha gari, akageuza gari na kuondoka eneo hil la hospitalini.
“Za muda Dany?”
“Safi tu”
“Ulikuja kumuona nani?”
“Ahaa kuna rafiki yangu nilikuja kumuona, kidogo malaria inamsumbu”
Nilimdanganya binti huyu na wala sikuhitaji aweze kunifahamu kwamba mimi ni nani.
“Ila anaendeleaje?”
“Yupo vizuri kiasi, siku mbili hizi watakwenda kumruhusu”
“Pole yake, ehee vipi unaelekea wapi kwa sasa?”
“Kusema ukweli kwa sasa sina pa kuelekea, ndio maana nikaona nikupigie ili kuweza kuonana na wewe tuzungumze”
“Kweli huna pa kuelekea Dany?”
 
“Yaa sina pa kuelekea, labda upange wewe”
“Okay, mmmmm…….tuelekee Tanga beach resort”
“Hakuna shaka katika hilo”
Binti huyu akaonyesha furaha kubwa aliyo kuwa nayo, sikujua lengo lake kubwa haswa ni nini, japo akili zangu zinanipekeka kwamba amenipenda kimapenzi japo sina uhakika sana katika hilo.
“Hivi unaitwa nani  vile?”
“Radhia, ila mara nyingi sana huwa wananiita Cajol”
“Basi na mimi nitakuita Cajol”
“Sawa upendavyo wewe”
Tukafika kwenye hoteli hii iliyopo pembezoni mwa bahari. Tukatafuta sehemu iliyo tulia kisha tukaketi. Kila mmoja akakaa kimya kwa dakika kadhaa akisubiria mwenzake aweze kuzungumza. Cajol akabaki akiwa anatabsamu tu, muhudumu akafika sehemu tulipo.
 
“Msikilize kaka hapo”
Cajol alizungumza huku akinitzama usoni mwangu, muhudumu akanitazama.
“Muna chakula gani?”
Akanipatia kkitabu kilicho andikwa idadi ya chakula kilichopo katika hii hoteli, nikakisoma taratibu kisha nikamuonyesha ni chakula gani ninacho kihitaji. Nikamuagizia na kinywaji ambacho ni kilevi hadi Cajol akanitazama.
“Unatumia kilevi?”
“Mara moja moja tu”
“Okay na mimi niletee kinywaji kama alicho agiza yeye”
“Je chakula”
“Hicho hicho kama chake”
Muhudumu akaondoka na kutuacha tukiwa tunatazamana, nikayatazama mandhari ya hili eneo, yananikumbusha kipindi nilipo kuwa na mama alipokuwa anatafutwa na majambazi wa meya wa jiji.
 
“Mbona unalishangaa lile eneo pale?”
“Ahaa…linanikumbusha mbali sana”
“Ulisha wahi kuja na mpenzi wako hapa nini?”
“Hapana, nilikuja na mama yangu, ambaye kwa sasa ni marehemu”
“Ohoo pole sana Dany, hata mimi mama yangu kwa sasa ni marehemu”
“Pole na wewe”
“Asante. Dany kusema kweli siamini kwenye maisha yanagu kama leo hii nipo na wewe, kwa maana ni kwa kipindi kirefu sana nilikutafuta ila sikuweza kukuona”
“Ni mihangaiko ya hapa na pele ndio ilinifanya niwe bize sana”
“Pole sana, Dany nahisi kwamba unaweza kunishangaa kwa kile ambacho nitakwenda kukizungumza”
Muhudumu akafika kwenye meza yetu na kutufanya tukatishe mazungumzo yetu, akatuwekea vinywaji tulivyo muagiza.
 
“Karibuni, chakula kinakuja muda si mrefu”
“Asante”
Muhudumu baada ya kuondoka, Cajoli akaendelea kuzungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Dany ni aibu kwa mtoto wa kike kuweza kuweka hisia zake za mapenzi mbele ya mwanaume, ila kwangu ninaomba niweze kuweka hivyo kwa maana kuseme kweli ninakupenda kutoka moyoni mwangu, na hilo jambo hadi baba yangu analifahamu, na nilikataa wanaume kadhaa ambao walipanga kunioa.”
Nikajikuta nikishusha pumzi huku nikimtazama Cajoli usoni mwake.
‘Masikini weee, laiti angejua moyo wangu kwa sasa hauna mapenzi ya kweli kwa mwanamke, wala asinge zungumza hichi anacho kizungumza’
 
Nilijisemea kimoyo moyo, huku nikimtazama Cajoli, sikuhitaji kuyakwepesha macho yangu usoni mwake, kwa maana ninahitaji kufahamu kama ni mkweli au ni muongo. Machozi yakaanza kumlenga lenga Cajoli hadi nikabaki nikkiwa ninamshangaa.
“Dany nilijipangia kukaa kwa miaka kumi ndio nije kukubali kuwa kimapenzi na mwanaume tofauti na wewe, kwa maana ningefahamu kwamba umekufa au upo mbali na sehemu nilipo mimi na ingebaki kuwa kama ndoto tu kwamba nimekutana na mwanaume ambaye nilimpenda ila sikuweza kumueleza kile ambacho nipo nacho moyoni”
“Cajol”
 
“Mmmmm”
“Unaniamini kitu gani hadi unanikabidhi moyo wako kwangu, ikiwa hunijui kama ni mkweli kwenye mahusiano au nimuongo”
“Danya kulifahamu au kuto kulifahamu hilo swala ni jambo ambalo wala halite niumiza moyo wangu, kikubwa ni kuweza kufahamu kwamba nimekupata wewe. Tazama sasa ni mwaka wa nne huu nimekuwa nikikusubiria wewe huoni ni…….”
Cajoli akanyamaza baada ya muhudumu kufika katika hili eneo. Akakiweka chakula mezani, akatukaribisha na kuondoka.
“Cajoli utakubali kuwa na mimi katika hii halia mbayo nipo nayo”
“Dany hali yako mimi sinto ijali, sinto jail kama ulikuwa unatafutwa na askari au laaa”
 
Nikastuka kidogo baada ya kugundua kwamba mimi nilikuwa nikisakwa na askari Tanza nzima, ila ni miaka michache iliyo pita nyuma.
“Nilikuwa nikikuombea kila siku, nilikuwa nikihakikisha kwamba haipiti siku ninakuombea mwenyezi Mungu kuweza kukulinda na mikasa yote hiyo ambayo unapitia na wala sikuwahi kumuambia mtu yoyote kwamba mwanaume ambaye ninampenda ni gaidi ambaye anatafutwa na serikali, japo nilijaribu kutembea kwenye mikoa ambayo nilihisi ninaweza kukupata ila sikufanikiwa”
Maneno ya Cajoli yakanifanya nizidi kuwa mpole, kati ya wanawake ambao nilisha wahi kuwa nao sikuwahi kusikia mwanamke hata mmoja ambaye anasema kwamba aniombea ili niwe wake.
 
Nikiwa katika kutazama tazama watu wanao ingia katika eneo hili, nikamuona Yudia akikatiza kwenye moja ya bustani ya hii hoteli akiwa ameongozana na jamaa wawili walio valia suti nyeusi, nikataka kunyanyuka kumfwata ila Cajoli akaniwahi kunishika mkono, akanyanyuka na kunikumbatia kwa haraka na kuanza kuninyonya denda, na kuniziba sura yangu kwa kupitia jicho langu la upande wa kushoto, nikamuona Yudia akisimama na kunitazama kwa macho makali sana jambo lililo nifanya nizidi kumnyonya denda Cajoli huku nikiiziba sura yangu kwenye uso wa Cajoli ili Yudia na watu wake wasije kuanzisha varangati nikiwa na huyu binti wa watu ambaye sihitaji matatizo yangu niliyo nayo yamkumbe yeye kama yaliyo mkuta Linda ambaye kwa sasa yupo mochwari.
                                                                           
AISIIIII……….U KILL ME 98                                                                                                

Yudia na watu wake wakaondoka, na kunifanya nimuachie Cajoli ambaye tayari alisha anza kulainika kwa jinsi ninavyo mnyonya denda.
“Nisubirie mara moja”   
“Unakwenda wapi Dany?”
“Ninakuja mara moja usiondoke”
“Sawa”
Nikaanza kutembea kwa mwendo wa haraka kuelekea sehemu alipo kwenda Yudia. Nikatoka hadi nje ya hoteli na kuona gari aina ya Toyota VX V8 likiondoka katika eneo hili la hoteli, nikazitazama namba zake za usajili na kuzikremisha.
“Samahani dada hili gari lililo toka wamepanda watu wangapi?”
Nilimuuliza muhudumu wa hii hoteli ambaye nimemkuta kipindi ninatoka nje.
“Wamepanda watatu, mdada mmoja na wengine ni wanaume”
“Shukrani sana, huwa wanapendaga kuja hapa?”
“Hapana ndio kwanza ninawaona leo”
Asante dada yangu”
Nikarudi sehemu nilipo muacha Cajoli, nikavuta kiti na kukaa.
“Mwenzio nimesha anza kula”
“Hakuna tabu, ehee niambie”
“Safi, natamani tukitoka hapa twende kwangu”
“Hilo halina tatizo kabisa”
“Kweli Dany”
“Yaa”
 
“Yaani sitamani hata kula hichi chakula naomba twende sasa hivi nyumbani kwangu”
“Tumalizie kula kwanza”
Tukaendelea kula haraka haraka, hadi tukamaliza kula. Tukamuita muhudumu aliye tuhudumia, Cajol akamlipa kiasi cha garama zote wanazo tudai, kisha tukaondoka eneo hili la hoteli.
“Mimi ninaishi maeneo haya haya ya hapa Sahare”
“Ahaa”
“Yaa kwangu sio mbali sana na hapa”
Cajol aliendelea kuzungumza huku akiendesha gari lake. Tukafika kwenye moja ya nyumba yenye geti kubwa, akapiga honi, geti likafunguliwa na mlinzi. Taratibu akaingiza gari lake ndani na kulisimamisha kwenye maegesho yaliyomo ndani ya hii nyumba yake.
“Dany karibu sana hapa ndio kwangu”
“Asante”
Cajol akatoa funguo kwenye pochi yake na kufungua mlango wa kuingilia ndani.
“Dany karibu jisikie upo kwako kabisa, na kuwa na amani”
“Asante”
 
Kitendo cha Cajil kufunga mlango wake wa mbele, akanikumbatia kwa nguvu na kuanza kunionya midomo yangu. Sikuwa na hiyana kabisa zaidi ya kuanza kumburudisha Cajoli binti kiarabu. Ndani ya muda mchache tukajikuta tukiwa tumezama kwenye dimbwi moja kubwa sana la mapenzi. Kila mmoja akajitahidi kwa uwezo wake kuhakikisha kwamba anamburudisha mwenzake.
“Dany nakupenda sana mwanaume wa ndoto zangu”
“Ninakupenda pia”
“Kweli Dany?”
“Ndio”
Majibu yangu yote hayana ukweli kwa maana kwa maisha yangu ya sasa sina upendo wowote moyoni mwangu, kwa maana nipo katika kipindi kikubwa sana cha kuweza kuwakabili maadui zangu ambao ndio kwanza nao ninahisi kwamba wanaaza kuniwinda. Cajoli akanikumbatiwa kwa nguvu huku machozi yakimwagika.
“Dany nakupenda sana, sihitaji kuwa mbali na wewe kwenye haya maisha yangu”
“Usijali kwa hapa nilipo fikia nitahakikisha kwamba ninakulinda na kukuheshimu, sinto hitaji adui yoyote kuweza kukushika wala kukudhuru”
 
Nilizungumza maneno ambayo sikufahamu hata yametokea wapi, machozi taratibu yakanza kunimwagika, si kwamba ninampenda Cajoli ika nikutokana na kuikumbuka familia yangu. Taratibu nikamuachia Cajoli na kujipangusa machozi yangu usoni.
“Una laptop?”
“Yaa ninayo”
“Unaweza kunisaidia pamoja na adapter, nikaweka memory card?”
“Ndio ninavyo njoo huku”
Tukaingia chumbani kwa Cajoli, nikiwa nimeishika shuruali yangu mkononi. Nikaitoa memory card ambayo nilikabidhiwa na Linda. Cajoli akaniwashia laptop yake na kunikabiza adapter ya kuwekea memory card. Nikaiweka, hazikupita sekunde nyingi, adapter ikasoma nikakutana na faili moja lililo andikwa kwa maandishi makubwa yanayo someka ‘SIRI’. Cajoli akanitazama usoni mwangu.
 
“Ngoja nikupishe ufanye kazi yako”
“Sawa”
Cajoli akaingia bafuani na kuniacha chumbani, nikafungua faili hili na kukuta video tatu pamoja na faili moja ambalo limeifadhiwa maandishi kadhaa. Nikafungua faili hilo na kuanza kulisoma taratibu.
‘Hii ni siri ambayo ni kubwa katika maisha yangu, kwa jina ninaitwa Linda Jonson, mimi ndio mtu ambaye nimehusika na kumficha mke wa makamu  wa raisi Eddy Godwin. Nilipewa kazi ya kumuua Phidaya na K2 kwa ajili ya wivu wake wa kimapenzi kwa kiongozi huyu.’
 
Nikajikuta nikimeza mate huku nikikaa vizuri kwenye kitanda nakuendelea kuisoma story hii.
‘Sikuwa ni mwanamke mwenye roho mbaya kwa maana niiye agizwa kumuua ni mwanamke mwenzangu. Kazi hii nilipewa na mwenzangu kwa jina anaye itwa Mariam. Mariam alipewa kazi ya kumua aliyekuwa mkuu wa mkoa Bi Joyce pamoja na familia yake.’
Nilijikuta nikistuka huku nikikaa vizuri kuendelea kuisoma stori hii ambayo sasa ninaanza kuupata ukweli kwa nani ni muhusika wa mauaji ya familia yangu.
‘Mariam aliweza kutekeleza azimio lake ambalo aliweza kuwepea, alifanya hayo yote kwa shinikizo la kuyalinda maisha ya mama yake. 
 
Wahusika wakuu katika kuwateka na kuwatumikisha mabinti wadogo katika meli kubwa iliyopo katikati ya bahari ni K2, ambaye kwa sasa yupo mbioni katika kinyang’anyiro cha kuwa raisi. Msaidizi wake mkuu ni Yudia, ambaye ni adui yangu mkubwa sana. Wa tatu ni Livna Livba huyu ni mkuu wa kikosi cha kuongoza wasichana wote wanao patikana kwenye gereza hilo’
Mapigo  ya moyo kwa mbali nikaanza kuyasikia yakinienda kasi. Sikutaka kuendelea kusoma maelekezo mengine, nikafungua video moja na kuanza kuona mandhari ya ndani ya meli hiyo ambayo ndipo walipo kusanywa wasichana wengi kutoka mataifa mbali mbali.
Nikafungua video nyingine, video hii inaonyesha jisni mama yangu aliyo kuwa akijitahidi kupambana na Mariam katika nyumba ambayo wala sielewi ni nyumba ya wapi. Mariam akafanikiwa kumtuliza mama yangu na kumchinja kabisa shingo yake. 
 
Machozi yakaanza kunimwagika usoni mwangu, yaliyo changanyikana na hasira kali. Mauaji hayo hayakuishia kwa mama yangu yakendelea hadi kwa Asma, Diana na mwanangu wa kike. Matukio yote haya yamerekodiwa na kamera za ulinzi zilizopo kwenye eneo hilo la mauaji.
“Dany”
Nilisikia sauti ya Cajol akiniita pembeni yangu, nikamtazama huku machozi yakiendelea kunimwagika usoni mwangu. Taratibu akanisogelea na kukaa pembeni yangu.
“Hawa ni kina nani?”
“Hii ni familia yangu, yote imesha uwawa”
“Mungu wangu, ndio wameuwawa kikatili kiasi hichi?”
“Yaa. Cajoli mwanaume ambaye upo naye sidhani kwamba ni sahihi kwenye maisha yako”
 
“Noo Dany, mimi nimerdhika na wewe, sijalishi kwamba wewe ni gaidi, au laa. Mimi ninakupenda na ninakuhitaji kwenye maisha yangu. Nitakusaidia kwa chochote kila ambacho utasema nikusaidie”
“Cajoli wakati nilio kuwa nao kwa hivi sasa ni mgumu sana, ni wakati ambao ninaweza kukuingiza wewe kwenye matatizo, sihitaji kukupoteza na wewe, sihitaji kukuona damu yako inamwagika pasipo kuwa na kosa lolo……”
Cajoli akaniziba mdomo wangu kwa kutumia kidole chake.
“Dany sijalishi nitamwagikwa na damu, sijali hilo, ninacho kihitaji ni kuhakikisha kwamba unashinda, unakuwa na furaha. Mimi nina pesa, mimi ninajuana na watu wengi, ninaweza kufanya chochote kupitia pesa yangu”
“Cajoli pesa katika hili aihitajiki, kwa maana watu wote ambao ninakwenda kukabiliana nao ni watu wenye nguvu kubwa sana hapa nchini, mmoja wao akiwa ni raisi huyu mpya wa hii nchi”
 
“Haijalishi Dany, mimi najua kitu cha kufanya, wewe niambie ni nini ambacho unakihitaji kwa sasa hivi”
“Ninacho hitaji ni kuanza kumsaka mtu mmoja baada ya mwengine nikiwa peke yangu, kama ni kunisaidia sihitaji ujulikane kama unanisaidia, kwa maana wakirudi kwako ni lazima watakuua”
“Sijali hilo Dany nitahakikisha kwamba kila jambo linakwenda vizuri mpenzi wangu”
“Sasa hivi ni saa ngapi?”
“Saa nne kasoro usiku”
“Ninaweza kupata wapi silaha”
“Silaha ya aina gani?”
“Bastola”
“Ninayo bastola yangu ambayo ninaitumia kwenye ulinzI binafsi”
“Unaweza kunipatia”
“Yaa”
Cajol akafungua kabati lake la nguo na kutoa bastola yake. Akanikabidhi, nikaikagua bastola yake na kukuta ina risasi za kutosha.
“Kwenye laptop yako ninaweza kuangali ni wapi ninapo weza kupata gari fulani”
 
“Yaa ninaweza kukufanyia hivyo”
Cajol akachukua  laptop yake, nikamtajia namba ambazo nilizikremisha kwenye gari alilo ondoka nalo Yudia na watu wake.
“Ina search”
“Nimelipata, kwa sasa lipo maeneo ya Mkonge hoteli”
“Nahitaji kwenda sasa hivi”
“Muda huu?”
“Ndio, kuna kazi ninahitaji kwenda kuifanya, nikitoka hakikisha unafunga milango na usifungue hadi pale nitakopo rudi”
“Sawa”
Nikaingia bafuni na kuoga kwa haraka kwa ajili ya kutoa jasho la mapenzi, nikarudi chumbani na kumkuta Cajoli  akiwa ameniandalia nguo zangu  ambazo nilikuwa nimezivaa, ila akaniongezea na sweta mbalo lina kofia yake kwa juu. Nikavaa nguo kwa haraka haraka, nikavaa na sweta hili, baada ya kuhakikisha kwamba nipo vizuri, nikaagana na Cajoli.
 
“Dany chukua simu hii nitakuwa ninakupa maelekezo kama gari hilo linaweza kuondoka katika hoteli hiyo”
“Sawa”
Nikachukua simu nyingine ya Cajoli, akanikabidhi na funguo za gari lake kisha nikaondoka. Safari ya kuelekea katika hoteli ya Mkonge hoteli haikuchukua muda mrefu nikafika, nikasimamisha gari kwenye maegesho, simu ya mfukoni mwangu ikaita ikanibidi kuitoa simu na kuipokea huku nikiwa nimesimama pembeni ya gari langu.
“Dany umefika”
Niliisikia sauti ya Cajoli akizungumza kwenye simu, ila kabla sijajibu nikahisi kitu kizito kikinigandamiza kichwani mwangu huku nikisikia sauti nzito ya mwanaume ikiniamrisha kwamba nisigeuke nyuma la sivyo atanichangua ubongo wangu.

==>>ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments