AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 95 na 96 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA           
Macho yangu yakawa yanacheza na saa ya ukutani, nikatamani masaa yasimame na nesi Linda aweze kufika, ila mawazo yangu sio sheria ya kufanya masaa wala dakika kuweza kusimmaa. 


Hadi inatimu saa nne usiku nesi Linda hajatokea, hata chakula ambacho huwa ninaletewa saa mbili na nusu usiku, sijaletewa. Nikajikuta nikinyanyuka kitandani kwangu, nikapiga hatua hadi mlangoni, taratibu nikaufungua mlango na kuchungulia nikaona askari wa ulinzi wakiranda randa kwenye kordo wakiimarisha ulinzi katika hii hospitali, jambo lililo nikatisha tamaa kabisaa ya kutoroka katika hii hospitali.

ENDELEA
Sikuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kurudi chumbani kwangu na kujitupa kitandani.
“Pisssss…….”
Nilisikia sauti ikitokea dirishani, kwa haraka nikanyanyuka kitandani.
 
“Zima taa”
Sauti ya nesi Linda niliisikia ikitokea dirishani, kwa haraka nikawahi kwenye swichi na kuzima taa ya chumbani kwangu. Nikafungua dirisha langu ambalo ni la kioo, nikachungulia nje, nikamkuta nesi Linda akiwa amevalia mavazi meusi huku  akiwa amejibanza kwenye ukuta na nisehemu ndogo sana amekanyaga katika ukuta huu.
“Ni muda wa kuondoka sasa”
Alizungumza kwa sauti ya chini huku akiendelea kuniangalia, nikabaki nikiwa nimemkodolea macho kwa maana sikujua ana ujuzi kiasi gani unao mfanya kuweza kufanya anacho kifanya.
“Dany ni muda wa kuondoka sasa unashangaa nini?”
“Po…poa poa “
Nikachungulia chini, japo kuna umbali, ila sikuwa na jinsi zaidi ya kufanya kama anavyo fanya nesi Linda. Taratibu nikatoka kwenye dirisha kwa umakini wa hali ya juu. Uzuri kwenye madirisha haya ya hospitalini hayana nondo ambazo zinaweza kumzuia mtu anapo hitaji kutoka. Nikasimama vizuri kwenye kijisehemu kidogo ambacho ni cha kukanyagia, huku mikono ikiwa nimeigandamiza vizuri kwenye ukuta.
 
Kwa mwendo wa taratibu tukaanza kutembea kuelekea kwenye dirisha la chumba kingine. Baada ya kufika katika dirisha hilo, nesi Linda akaingia, kisha nikafwatia mimi. Akawasha tochi kubwa ambayi sifahamu ameitoa wapi. Nesi Linda akanifwata na kunikumbatia kwa nguvu huku akihema kwa pumzi nzito ya mahaba.
“Dany hatuna muda wa kukaa hapa, niwakati wa kuondoka sawa mpenzi wangu”
“Sawa ila chumba hichi ni cha nini?”
“Hii ni stoo ya nguo za madkatari, sasa ni muda wa kuvaa nguo haraka haraka”
“Poa”
Nesi Linda akaanza kumulika baadhi ya makabati, akanitolea nguo za kidaktari pamoja na vitambaa malumu wanavyo jifunga kwenye midomo pamoja na pua zao kipindi wanapo kwenda kufanya upasuaju. Alipo hakikisha kwamba nimemaliza kuvaa nguo hizo na kukivunga kitambaa hichi chenye rangi ya kijani vizuri.
 
“Kuna viatu hivi vaa”
Nikavaa viatu hivyo, akanipatia kitambulicho nikakivaa shingoni kamba yake na kikaning’inia kifuani. Nesi Linda naye akamalizia kuvaa mavazi ya kidatkari, taratibu akausogelea mlango akachungulia nje.
“Dany njoo”
Nesi Linda aliniita kwa sauti ya chini, taratibu nikamfwata hadi sehemu alipo. Akazima tochi kisha taratibu tukatoka chumbani humu. Tukaanza kutembea kwenye kordo hii kwa kujiamini sana. Tukapishana na walinzi pasipo kusemeshana nao na kila mlinzi hakuwa na shaka na sisi kabisa. Tukaelekea maeneo ya maegesho ya magari, nesi Linda akaingia kwenye gari la wagonjwa na mimi nikaingia ndani ya gari hilo.
 
“Pale getini si kuna ukaguzi?”
“Hilo niachie mimi nitajua nini cha kufanya”
Tukatoka na gari la wagonjwa taratibu hadi getini. Kama kawaida askari wa getini wakaanza kutukagua.
“Tunakwenda kumchukua mgonjwa nyumbani kwake tumepigiwa simu ni dharura”
“Ohoo sawa dada munahotaji usindikizaji wa askari?”
“Hapana kaka sio mbali na hapa tunakwenda kumchukua mgonjwa”
“Sawa dada”
Nesi Linda akarudisha kitambaa chake usoni, akapandisha kioo cha gari na kuondoka eneo hili la hospitali pasipo walinzi kuweza kunistukia kwamba mimi niliye kaa pembeni sio daktari.
“Mbona imekuwa kirashisi hivyi tofauti na hata nilivyo kuwa nimefikiria”
“Ahaa hao ninawajua mimi, laiti tungetumia gari la kawaida, ingekuwa ni shida sana kwetu, kwa maana wangehitaji hata wewe kuvua kitambaa chako usoni”
 
“Shukrani sana Linda, kwa maana nilikuwa ninatamani sana kutoka katika ile hospitali ila nikawa ninashindwa”
“Kwa nini ulitaka kutoka, wakati upo pale kwa ajili ya matibabu?”
“Ni mambo mengi sana tukikaa na kutulia tutayazungumza vizuri”
“Usijali kuna sehemu nimeacha gari langu hapo”
“Na hili gari vipi?”
“Tutaltelekeza”
“Huoni kwamba unaweza kuisababisha kazi yako kuingia katika matatizo”
“Yaani mimi hapa Dany nimesha acha kabisa na ndoa sitaki tena”
“Eheee”
“Ahaa sasa unahisi ninaendelea kukaa kwenye ndoa kufanya nini wakati raha y ambo** siipati”
“Heee!!”
“Shangaa tu, ila Dany umenipa kitu ambacho sikuwahi kukipata katika maisha yangu, sijali ni kitu gani ambacho kinaweza kutokea kwenye maisha yangu ila ukweli ni kwamba umenichanganya kabisa, sioni wala sisikii”
 
Linda alizungumza huku akiongeza mwendo kasi wa gari lake. Tukafika kwenye moja ya kona, akasimamisha gari.
“Tushuke”   
“Ila hapa ni kwenye kona”
“Yaaa tushuke”
Tukashuka kwenye gari, pembezoni mwa barabara kuna korongo moja refu.
“Gari  naliweka free nalisukumia huko”
Linda alizungumza kwa kujiamini, akatafuta jiwe lenye uzito kiasi, akaliweka sehemu ya kukanyagia mafuta wakati wa kuendesha gari. Taratibu gari likaanza kusogea mbele akalikatisha kona kwa kutumia mskani huku akiwa nje. Gari likaanza kushuka kwenye korongo hilo na kuangukia chini. Tukaanza kuingia kwenye msitu na kuanza kutembea kwa kujiamini.
“Tunaelekea wapi?”
“Hapa tunavuka boda la Kenya na Tanzania, gari langu nimeliacha huko Tanzania ndio maana unaweza kuona kwamba nilichelewa kufika kukuchukua”
 
“Sasa sawa, ila nikuulize kitu Linda”
“Niulize”
“Kabla ya kuwa nesi ulishawahi kufanya kazi gani?”
“Daaa ni story ndefu sana ila tuvuke huu mpaka ndio tutazungumza”
“Poa”
Mwanga wa mbalamwezi unatusaidia kuona tunapo elekea, japo ni porini kubwa tunalo likatiza ila hakuna ambaye ana wasiwasi, lengo letu kubwa ni kuweza kufika sehemu ambapo Linda ameliacha gari lake. Tukafanikiwa kufika katika sehemua mbayo Linda ameliacha gari lake aina ya Toyota VX V8.
“Kuna nguo nilizichukua zipo huku nyuma ya gari itabidi kubadilisha”
“Poa”
Linda akafungua gari lake kwa nyuma, na kweli nikakuta nguo kadhaa pamoja na begi moja juesi, sikujua linakitu gani ndani yake, na wala sikuhitaji kujishuhulisha kuweza kufahamu kwamba lina kitu gani. Tulipo hakikisha tumebadilisha mavizi yetu tuliyo kuwa tumeyavaa, tukaanza safari ya kulitafuta jiji la Arusha huku mimi nikiwa ni dereva kwa maana nina ufahamu vizuri mkoa wa Arusha na barabara zake.
“Tupumzikie Arusha?”
“Hapana nilikuambia kwamba mume wangu yupo hapa kikazi, so inaweza ikatokea bahati mbaya tukakutana naye ikawa ishu”
 
“Sawa”
Saa iliyopo kwenye gari inatuonyesha ni saa tisa usiku. Safari ikazidi kusonga mbele hadi inatimu saa kumi na moja alfajiri, tumefika Mombo.
“Dany upo vizuri katika kuendesha gari”
“Asante”
“Laiti ingekuwa ni mimi wala tusinge kuwa hapa, ndio kwanza tungekuwa nyuma huko”
“Uzuri wa gari lako lina uwezo wa kuhimili mwendo  kasi”
“Kweli eheee?”
“Yaaa, sasa tunaelekea mkoa gani kwa maana sasa, tupo mkoa wa Tanga?”
“Dany mimi nakusikiliza wewe tu yaani popote mimi nitakwenda”
Sikuona jaya ya kwenda mkoa wa mbali tofauti na Tanga, moja kwa moja nikaelekea Tanga mjini, ambapo tukafika katika hoteli moja iitwayo Nyinda, ambapo tumefika majira ya saa mbili asubihi, na ndio kwanza baadhi ya watu wanatoka kwenye hii hoteli kuendelea na maisha yao.
 
“Dada habari?”
“Salama vipi kaka”
“Safi, ninaweza kupata chumba”
“Yaa vipo, vimebaki vyumba vya V.I.P ni shilingi elfu stini kwa siku”
Ikanibidi kumgeukia Linda kwa maana hapa nilipo sina hata senti tano.  Linda akafungua pochi yake ndogo na kutoa kibunda cha elfukumi kumi za kitanzania, akanikabidhi.
“Nitalipia kwa siku nne ni kiasi gani?”
“Laki mbili na arobaini”
Nikahesabu kiasi anacho kihitaji huyu muhudumu, nikampatia kiasi hicho. Akatukabidhi funguo za chumba, akatupa maelekezo ni wapi chumba kilipo, nikalibeba begi jeusi la Linda na kueleka katika chumba chetu. Tukaingia na kufunga mlango kwa ndani, kwa haraka Linda akanifwata na kunikumbatia kwa haraka. Tukaanza kunyonyana midomo yetu, huku kila mmoja akiwa na hamu ya kupata penzi la mwenzake. 
 
Ndani ya dakika moja kila mtu nguo zake zikawa hazipo mwilini. Nikambeba juu juu Linda na kumuweka juu ya dreasing table kubwa iliyopo katika hichi chumba. Mikono yetu ikawa na kazi ya kukatiza kila sehemu ya miili yetu. Taratibu tukaianzisha safari ambayo Linda anaifurahia sana, sikuwa na hiyana zaidi ya kuhakikisha kwamba ninampa Linda kile anacho stahili kukipata kwa muda huu.
Mchezo ukamalizika, Linda akiwa anafuraha sana, tukaingia bafuni kuoga kwa pamoja na kurudi chumbani.
 
“Dany kwa nini ulitaka kuondoka pale hospitalini”
Swali la Linda likanifanya nimsogelee kitandani alipo kaa, nikakaa pembeni yake huku nikimtazamaa usoni mwake. Sikuhitaji kumuamini sana kwa maana kidonda cha kumuamini Livna bado hakijapona moyoni mwangu.
“Unajua kwenye maisha yangu sijazoea sana kuishi maisha ya kukaa ndani sehemu moja huwa siyapendi”
“Ahaa, ilikuwaje ikaletwa pale ukiwa na majeraha mengi mwilini mwako?”
“Nilitekwa na majambazi, wakanitesa hata na fika pale hospitalini kwenu sikumbuki hata ilikuwaje”
“Pole sana mpenzi wangu sasa kwa nini walikuteka?”
“Ahaa kuna siri yao moja walihisi kwamba ninaifahamu, ila kusema kweli sikuwa nina ifahamu kabisa. Vipi kwa upande wako?”
Mimi nilikuwa ni mmoja wa mabinti ambao nilikulia katika maisha ya kikamanda”
“Kivipi?”
 
“Nilipo kuwa mdogo niliweza kuchukuliwa na kupelekwa kwenye kambi moja, ambayo huko tulikuwa tunaishi watoto wa kike pekee. Ni kambi ambayo kazi yetu tulikuwa tunafundishwa kuua na kuwa na roho mbaya, nilipo bahatika kupata nafasi ya kutoroka katika kambi hiyo, basi niliweza kujichagulia maisha ya kuwa daktari”
“Hiyo kambi yenu ilikuwa wapi?”
“Kusema kweli hata mimi sifahamu kwamba ilikuwa wapi, ila tulikuwa tupo kwenye meli kubwa na katikati ya bahari”
Historia ya Linda inaendana kabisa na Mariam pamoja na Livna Livba. Sikutaka kujionyesha kama ninafahamu kitu chochote katika histori yake. Linda akasimama kwenye kitanda na kuanza kutembea kwa mwendo wa madoido huku akitingisha makalio yake. Akawasha Tv kisha akarudi kitandani nilipo kuwa nimekaa.
 
“Dany ninaomba unisaidie kitu kimoja”
“Kitu gani?”
“Ninahitaji kumuua raisi wa hii nchi”
“Unahitaji kumuu raisi wa Tanza!!”
Niliuliza kwa mshangao huku nikimtazama Linda usoni mwake, nikiwa ninajifanya mjinga mkubwa sana nisiye elewa ni kitu gani kinacho endelea.
“Ndio, nimekushirikisha hili swala ila ninakuomba usimuambie mtu wa ina yoyote, pia ninakuomba tushirikiane katika hili swala”
Moyoni mwangu nikajikuta nikijawa na furaha kwa maana mpango wangu unakwenda kukamilika, taratibu na kwa kumtumia Linda, nitakwenda kulipiza kisasi changu cha kimya kimya pasipo mtu yoyote kuweza kunistukia.

AISIIIII……….U KILL ME 96                                                                                                


“Siwezi kumuambia mtu wa aina yoyote. Ila ni kwanini unataka kumuua raisi?”
Niliuliza kuweza kumfahamu Linda vizuri.
“Raisi kuna mamb mengi ambayo amenifanyia kwenye maisha yangu moja wapo likiwa ni kuiangamiza familia yangu”
“Eheee, hembo ngoja mara moja, unataka kuaniambia raisi ameweza kuua familia yako?”
“Yaa kipindi walipo  kuwa wananichukua, kunipeleka katika kambi yake ya mafunzo, baba na mama yangu waliweza kuuwawa kikatili sana jambo ambalo hadi leo linausumbua sana moyo wangu na nilazima nilipize kisasi”
Taarifa ya ziara ya raisi mkoa wa Tanga, ikaanza kuonyeshwa kwenye Tv iluyopo humu ndani. Nikamuona K2 jinsi anavyo zungumza na wananchi huku maandishi madogo yakiandikwa kwa chini kwamba yeye ndio raisi wa hii nchi, jambo lililo anza kuniumiza kimya kimya moyoni mwangu. Sikuhitaji kumuonyesha Linda kwamba hata mimi nimejeruhiwa na K2, ambaye ninahisi ana maadui wengi kati hii nchi ya Tanzania.
“Nilazima kumuu huyu mwanamke”
Linda alizungumza huku akiyakaza macho yake kwenye Tv hii kubwa.
 
“Anakuja lini hapa Tanga?”   
“Wala sielewi, ila nitauliza uliza kuweza kufahamu kwamba ni siku gani ambayo anakuja”
“Dany fanya hiyo niweze kujua ni lini anakuja, tutatumia garama ya aina yoyote kuhakikisha kwamba mpango wetu unafanikiwa.”
“Sawa”
Nikachukua simu ya mezani, nikawasiliana na muhudumu na kumuagiza chakula. Linda akachukua begi lake jeusi na kuliweka kitandani. Akalifingua, ndani ya begi kuna baadhi ya nguo pamoja na silaha. Akatoa nguo na kuziweka juu ya meza, kisha akatoa bastola nne pamoja na magazine zake na kuziweka juu ya kitanda. Chini ya begi kuna pesa nyingi noti za Kenya, zilizo pangwa vizuri.
“Hii pesa inatutosha katika kuikamilisha kazi yetu”
“Ni kiasi gani?”
“Milion kumi za kenya”
“Nafikiri zitatosha, ila kuna jambo ambalo nimeliwaza”
“Jambo gani?”
 
“Leo nahitaji kuingia mtaani kwenda kufanya upelelezi mdogo kisha badae nitarejea na jibu, ni wapi na niwakati gani ambao raisi anakuja Tanga”
“Sawa, ila mimi utaniacha ndani?”
“Yaa hii kazi ninahitaji kuifanya peke yangu”
Mlango wa hapa chumbani kwetu ukagongwa, nikajifunga taulo kiunoni mwangu  kisha nikausogelea taratibu kwa umakini, nikaufungua. Nikamkuta muhudumu akiwa ameshika sinia kubwa lenye sahani mbili zenye chakula, nikakipokea chakula na kuufunga mlango.
“Chaku mbona kinanukia vizuri?”
“Ndio mambo ya kitanga hayo”
“Mmmm hadi kimenipa hamasa ya kula”
Linda alizungumza huku akinyanyuka kitandani, akanipokea chakula hichi na kukiweka mezani. Taratibu tukaanza kula huku kila mmoja akiwa katika hali ya furaha, japo ni masiano yaliyo anza kwa muda mfupi tu ila mimi na Linda tunajikuta tukiwa katika furaha ambayo kwa mara ya kwanza ukituona unaweza kuhisi labda tumeonana siku nyingi za nyuma.
 
“Honey mimi niahitaji kwenda kuianza kazi”
“Sawa, ila Dany ninakuomba usichelewe mume wangu”
“Sinto chelewa mke wangu”
Nikavaa nguo zangu ambazo nilikuwa nimezivaa jana usiku, nikachukua kiasi cha kutosha cha pesa za kikenya. Nikatoka nje ya hoteli, sikutaka kutumia gari la Linda kwa maana bado sijamfahamu vizuri, nikakodi taksi, nikamuagiza dereva anipeleke kwenye moja ya duka la kubadilisha pesa.
“Barabara ya kumi na mbili, kuna duka moja la kubadilisha peza za kigeni”
“Hakuna tabu, baada ya hapo nitahitaji unipeleke chumbageni”
“Sawa bosi”
Hatukuchukua muda mwingi sana tukawa tumesha fika katika duka hilo la kubadilishia pesa, nikashuka na kuingia ndani ya duka hili. Nikakutana na dada mmoja wa kiarabu.
“Habari yako dada”
 
“Salama tu”
Nilimsalimia dada huyu huku nikitoa noti kadhaa mfukoni mwangu, macho ya dada huyu wa kiarabu muda wote yakawa yananitazama usoni mwangu hadi nikaanza kujistukia.
“Ahaa ninabadilisha elfu mbili”
“Sawa hakuna tabu”
Nikamkabidhi dada huyu noti za kikenya, akaanza kuzihesabu kwa mashine maalumu, ila muda mwingi huyu dada macho yake anayatupia kwangu.
“Dada mbona unanitazama sana”
“Ahaa kuna kaka mmoja ninakufananisha na kaka mmoja hivi”
“Ahaaaa”
“Yaa kuna kaka mmoja kuna siku alinipa lifti akiwa na mwenzake nilicha na basi pale Lugoba, ni miaka mingi ya nyuma sijui kama utakuwa unakumbuka?”
 
Tukio la dada huyu likarudi kichwani kwangu haraka sana, nikakumbuka siku ambayo tuliweza kumpatia dada huyu lifti nilikuwa ninatoka Dar es Salaam nikiwa na dererva wa kampuni baada ya kupewa likizo na K2 kutokana na kupata na majeraha ya kuungua na moto.
“Ohooo ninakumbuka sasa”
“Ndio wewe?”
“Yaa za masiku?”
“Safi kaka yangu, aissee yaani nilijaribu kusubiria simu yako nione kama utanipigia ila sikuona chochote hadi leo”
“Ahaa kuna matatizo kadhaa ambayo yalitokea ndio maana nikawa bize kwa miaka mingi hiyo”
“Pole asieee,  sasa sijui  leo tunaweza kupata hata muda wa kuzungumza mimi na wewe”
Dada huyu wa kiarabu anaonyesha hali ya uchangamfu mkubwa sana kwangu, nikajifikiria kwa muda, nikijaribu kuupanga muda wangu kama ikiwezekana niweze kuonana naye kwa leo.
 
“Ahaa kwa leo ninaona ratiba yangu haipo vizuri dada yangu, labda kwa kesho”
“Tafadhali kaka yangu ninakuomba kwa leo”
“Kuna jambo muhimu ambalo unahitaji kuniambia?
“Ndio ni la muhimu”
“Unaweza kuniachia namba yako ya simu, nikakutafuta?”
“Kwa leo?”
“Yaa kwa leo”
“Ninaweza kukutajia hapo?”
“Ahaa sina simu kwa sasa”
“Ngoja nikuandikie”
Dada huyu akaniandikia namba zake kwenye kikaratasi na kunikabidhi, akanikabidhi pesa zangu. Nikaagana naye na kutoka nje, nikaingia kwenye gari.
“Twende sasa chumbageni”
“Sawa mkuu”
Nikaanza kumpa maelekezo dereva hadi kwenye nyumba ambayo tulikuwa tunaishi hapo zamani na mama yangu. Taratibu nikashuka kwenye gari huku mwili mzima ukiwa unanisisimka, nikajikuta nikipiga hatua hadi kwenye geti. Nikaunyanyua mkono wangu taratibu ili niweze kubisha hodi ila nikajikuta nikishindwa kubisha hodi. 
 
Gafla nikasikia mlipuko mkubwa ukitokea eneo la mbali kutokea katika sehemu hii, si mimi peke yangu ila kila mwananchi aliweza kustuka kutokana na mlipuko huo. Nikapiga hatua za haraka hadi karibu na gari nikatazama upande wa kaskazini ambapo ndipo mlipuko huo umetokea.
“Ni nini hicho?”
Dereva taksi aliniuliza huku akishuka kwenye gari akiwa katika hali ya woga sana. Moshi mwingi unao samba hewani uliniashiria kabisa kwamba mlipuko huo ni wa bomu.
“Twende kwenye hiyo sehemu tukashuhudie hilo tukio”
Nilimuambia dereva taksi, akatii amri yangu kama mteja wake, japo anawasiwasi mwingi ila kutokana anahitaji pesa ikambidi kufanya ninacho muelezea.
“Hasani, mlipuko umetokea wapi?”
Dereva taksi alizungumza na simu huku akizidisha mwendo kasi wa gari.
“Weeee imekuwaje?”
“Poa poa ninakuja”
 
Dereva taksi akakata simu huku akiiweka pembeni.
“Umetokea wapi mlipuko”
“Pale hoteli ya Nyinda tulipo anzia safari yetu”
“NINI?”
“Yaa hapo hapo”
Nilihisi kuchanganyikiwa kwa maana katika hoteli hiyo ndipo nilipo muacha Linda.
“Ongeza ongeza mwendo bwana”
Nilimuhimiza dereva kuendesha gari kwa mwendo wa kasi sana. Dereca akazidi kuongeza kasi hadi kila sehemu ambayo anapita ikamlazimu kupiga honi ilimradi watu waweze kumpisha. Tukafika kwenye hoteli, kwa haraka nikachomoa pesa mfukoni wala sikujua ni kiasi gani, nikampa dereva na kwa haraka nikashuka kwenye gari na kuanza kukimbilia sehemu ya tukio japo, watu wengi walipo katika hili eneo wanaudhurika na tukio hili la mlipuko wa bomu. 
 
Asilimia kubwa ya jengo hili la hoteli limebomoka, na watu wengi wamefariki. Hata mlango wa kuingilia ndani ya hii hoteli hauonekani. Nilijihisi kuishiwa nguvu, gari la zima moto likafika eneo la tukio, huku magari ya wagonjwa yakizidi kumiminika katika eneo la tukio.
“Usinishike”
Nilizungumza kwa hasira huku nikumsukuma mtu aliye nishika nyuma yangu, akili yangu yote kwa wakati huu inamfikiria Linda.
“Ondoka eneo la tukio”
Ikanibidi kugeuka na kutazama mwanaume huyu aliye valia mavazi ya askari wa zima moto. Nikamtazama kwa macho ya hasira sana ila akaendelea kunisisitizia kuondoka katika eneo la tukio. Taratibu nikasogea katika eneo hili la tukio ambalo bado moshi mwingi unaendelea kurindima katika eneo zima. 
 
Eneo la maegesho ya magari katika eneo hili, silioni gari  la Linda, jambo lililo anza kunipa wasiwasi kidogo, nikatembea hadi katika eneo ambalo nililisimamisha, sikuliona kabisa. Taratibu nikamfwata dereva mmoja wa bodaboda ambaye muda ambao nilikuwa niondoka hapa hotelini alikuwepo.
“Vipi kaka?”
“Safi”
“Imekuwaje hapa “
“Daa kuna gari moja nyeusi iliondoka hapa kwa kasi, tazikupita hata dakika mbili mlipuko ukatokea”
“Gari ya aina gani?”
“Gari moja aina ya V8, yale wanayo tembelea nayo wabunge”
“Aliondoka nayo nani?”
“Dada mmoja hivi mrefu kiasi, mweupe”
Huyo dada ambaye ananieleza huyu dereva bodaboda, hafananii kabisa na Linda, kwa maana Linda ni mweusi japo ni mrefu kiasi.
“Alitoka katika mazingira ya aina gani?”
“Alitoka anakimbia, tena kama picha nilimpiga kwenye simu yangu, yaani ni bonge la totozi”
Dereva bodaboda alizungumza huku akinipatia simu yake, nikaichukua na kuitazama picha hiyo. Sikuamini macho yangu baada ya kumuona Yudia kwenye hii picha akiingia kwenye gari la Linda, jambo  lililo nifanya nijikute nikianza kufura kwa hasira kwa maanaYudia na mwenzake na K2 bado wananiandama sana kwenye maisha yangu.

ITAENDELEA KESHO



from MPEKUZI

Comments