AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 116 na 117 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA     
 “Yudia, mbona una hatari sana?”   
“Kwa nini?”
“Yudia analindwa sana kuliko hata Hawa, na Yudia kwa sasa ana cheo kikubwa kuliko Hawa”
“Kisa ni nini cha Hawa kushushwa cheo ikiwa yeye ni mtoto wa mkuu”
“Kisa cha yeye kushushwa cheo na kupokonywa madaraka yote ni wewe Dany”
Nikabaki nikiwa nimekodolea macho mwalimu kwa maana nina kipindi kirefu sana tangu mimi kuondoka katika hii kambi na sijafahamu ni kitu gani Hawa amekifanya na kinacho nihusu mimi hadi kupokonywa madaraka yake na kukabidhiwa Yudia.
   
ENDELEA   
“Kisa mimi?”   
“Yaa, Hawa tangu ulivyo pata mateso na kufikia hatua ya baba yake kukuuza kwa watu ambao hawajulikani, ilimsikitisha sana Hawa. Akawa hafwati sheri inayo wekwa na baba yake, akawa ni msichana wa pombe. Ilifika hadi hatua baba yake akaamua kumuweka mahabusu”
“Nini?”
“Yaa huo ndio ukweli, hawa yule ambaye tulikua hatuifahamu sura yake, sasa hivi tunaiona kama kawaida”
Hapa ndipo nikaanza kupata picha kwenye video ambayo K2 alitumiwa na magaidi, nilimuona Hawa na baba yake, japo sikutilia maanani ni kwa nini aliruhusu sura yake kuonekana katika mkanda huo wa vidoe.
 
“Sasa hawa kwa sasa yupo wapi?”
“Yupo kwenye chumba chake, katika ile nyumba ndogo”
“Kwa hiyo ametolewa kwenye lile jumba kubwa”
“Yaa, yaani nikikuambia amepokonywa kila kitu ujue hana chochote, mipango yote kwa sasa anaiendesha huyo Yudia, hapa watu hatukaliki, kama ninasikia amefanya mashambulizi juzi Tanzania, na hadi hapo hakuna hata shambulizi moja lililo fanikiwa”
“Ticha unaweza kunisaidia jambo moja”
“Jambo gani Dany”
“Ninahitaji kwenda kumuona Hawa usiku huu”
Mwalimu akaka kimya kwa muda huku akitafakari ombi langu ambalo mimempatia
“Sawa twende, ila funga hicho kitambaa chako usoni”
“Sawa”
 
Nikafunga kitambaa changu na kubakisha sehemu ya macho yangu. Tukaanza kutembea kwa kasi kuelekea katika nyumba ndogo inayo sadikika kwamba ndipo alipo Hawa. Walinzi hawakuweza kunistukia kwa maana nipo kwanza na mwalimu wa hii kambi pili ninafahamu nyendo na mienendo ambayo Wasomali wengi huwa wanatembeaa, kwa hiyo hata tembea yangu ilinilazimu kuibadilisha kwa muda ili nisijulikane. Tukakutana na walinzi wawili wa kike nje la mlango wa nyumba hii
“Ninawaomba nionane na mkuu”
Mwalimu alizungumza huku akiwatazama walinzi hawa kwenye nyuso zao.
“Mkuu kwa sasa amelala”   
“Ninawaomba mumuamshe, muelezeni kwamba ni dharura. Tafadhali”
Walinzi hawa wakatazamana, kisha mmoja akamkonyeza mwenzake, akafungua mlango na kuingia ndani. Baada ya dakika moja akarudi.
 
“Amekuomba uingie”
“Nisubiri hapa”
Mwalimu alizungumza, nikatingisha kichwa, akaingia ndani na kuniacha na walinzi hawa huku nikitazama tazama mazingira ya eneo hili ambalo ninalifahamu vizuri sana na hakuna kitu chochote ambacho kimeweza kubadilika.
“Unaitwa ndani”
Mlimzi mwengine wa kike aliye toka ndani, alizungumza na mimi kwa lugha ya kiarabu ambayo ninaifahamu vizuri. Nikaingia ndani nikiwa na bunduki yangu, Hawa aliye kaa kwenye sofa baada ya kuniona kwa haraka akanyanyuka na kunikimbilia kwa harakana na kunikumbatia kwa nguvu.
“Ohoo asante Mungu, Dany upo salama”
 
“Hata mimi pia ninamshukuru Mungu kukuona upo salama”
Nikavua kitambaa changu huku tukiachiana na Hawa, akawatazama walinzi wake wengine wawili walipo humu ndani pamoja na mwalimu. Kisha akanishika mkono na tukaingia kwenye chumba chake cha kulala. Kitu cha kwanza tu baada ya Hawa kuufunga mlango, akanikumbatia kwa nguvu huku akiangua kilio  kikubwa sana japo ni cha chini chini, ila inaashiria kabisa kwamba analia kwa uchungu pamoja na maumivu ya muda mrefu yaliyo kuwa ndani ya moyo wake kwa muda mrefu.
 
“Shiiii usilie Hawa”   
“Dany hujui ni mateso ya kiasi gani ambayo nimepitia kwenye maisha yangu tangu kuondoka kwako katika hii kambi”
“Hawa sikuondoka kwa kupenda”   
“Yaa ninafahamu hilo Dany, samahani kwa kushindwa kukusaidia kipindi ulivyo pata matatizo”
“Yamaesha pita hayo”
Hawa akaniachia na kunitazama mwili wangu, machozi yakendelea kumwagika usoni mwake, ikabidi nimkumbatie tena na kukirudisha kichwa chake kifuani mwangu.
“Usilie Hawa nipo karibu nawe sasa”   
“Kweli Dany?”
“Yaaa, nimekuja kwa kazi moja tu”
“Kazi gani?”
“Nahitaji kumuua Yudia”
“Kwa nini?”
Swali la Hawa likanifanya nikae kimya huku nikimtazama usoni mwake kwa maana ninazielewa vizuri hisia za Hawa juu yangu na nikimumbia kwamba nilikuwa nina mke ninaweza kumjengea hali ambayo sihitaji kumjengea kwa muda huu. Pia Yudia amehusika katika mauaji ya Linda msichana aliye nisaidia kutoka katika hospitali niliyo kuwa nimepelekwa na John .
 
“Dany”   
“Yaaa”
“Yudia amekufanyia nini?”
“Yudia amefanya mambo mengi sana kwenye maisha yangu, nilimfahamu Yudia hata kabla hajakuja kwenye hii kambi. Yudia alikuwa mfanyakazi wa ndani nyumbani kwetu miaka mitatu nyuma”
“Mfanyakazi wa ndani?”
“Yaa alikuwa ni mfanyakazi wa ndan, ila pale nyumbani alikuja kwa kazi maalumu na baada ya muda niligundu ya kwamba ametoka katika kundi hili”
“Sijawahi kuisikia stori ya Yudia kuwa mfanyakazi wa ndani, ila hilo lisiniumize kichwa sana, kabla ya kufanya lililo kuleta ninakuomba unisaidie kitu Dany wangu”
“Kitu gani?”
 
“Ninahitaji kurudi kwenye madaraka yangu, ila sina mtu wa kunipa njia za mimi kuweza kurudi katika madaraka yangu niliyo pokonywa na Yudia”
“Kwani wewe na Yudia muna mahusiano gani kati yenu?”
“Ni ndugu, ila kwa sasa baba ametokea kumthamini sana Yudia kama vile ni mtoto wake wa kumzaa wakati ni baba mdogo kwa baba mkubwa”
“Hawa kama utahitaji msaada wangu, basi hakuna njia nyingine ya kufanya zaidi ya kuua?”
Hawa akaka kimya huku akinitazama usoni mwangu akiwa kama haamini kwa kile ambacho nimekizungumza.
“Hawa baba yako, Yudia hao wote kwangu ni maadui, pasipo kufanya mauaji hakuna kitu ambacho kinaweza kukurudisha wewe kwenye nguvu. Utaendelea kuwa chini na utaendelea kuwatumikia wao na watakuweka kwenye kifungo hichi cha ndani hadi mwisho wa maisha yako”
“Dany ninaogopa”
 
“Katika hili hakuna kuogopa, baba yako kama angekuwa anakupenda na kuheshimu mawazo yako, kwanza asinge fanya ukatili kama huu ambao amenifanyia, ilifikia hadi hatua akataka kukata uume wangu, so alihitaji kunihanisi?”
Nilizungumza kwa hasira ila kwa sauti ya chini huku nikimtazama Hawa usoni mwake. Hawa machozi yakaendelea kumwagika kwa maana kila kitu ninacho kizungumza ndicho kilicho jitokeza kwenye maisha yangu.
“Hawa wewe unahitaji nguvu, kwa nini tusitumie umoja wetu kuchukua madaraka kwenye hili kundi. Sihitaji kuwa muongo wala mnafki kwako, nikimua baba yako na Yudia, roho yangu itatulia”
 
“Noo Dany baba yangu hana la hatia katika mikono yako?”
“Unahitaji msaada wangu au auhitaji msaada wangu?”
Nilizungumza kwa sauti nzito huku nikimtazama Hawa usoni mwake, taratibu akakaa kwenye kitanda chake huku machozi yakimwagika, nikamsogelea na kusimama mbele yake, taratibu nikachuchumaa na kukinyanyua kichwa chake alicho inamisha uso wake chini.
“Hawa natambua ni jinsi gani unavyo mpenda baba yako, ila unatakiwa kuhakikisha kwamba tunafanya liwezekanalo kuhakikisha kwamba baba yako na Yudia wanaondoka kwenye uso huu wa dunia”
 
Hawa akaendelea kukaa kimya huku akimwagikwa na machozi, nikaupitisha mkono wangu wa kushoto na kuishika shingo yake kwa nyuma, taratibu nikamsogeza karibu na uso wangu, tukatazamana kwa sekunde kadhaa. Uvumilivu ukatushinda na kutufanya tuanze kunyonyana midomo yetu kwa kasi sana huku kila mmoja akiwa anatoa mihemo mizito ya mahaba. Galf tukasikia king’ora cha tahadhari kilichotufanya mimi na Hawa kuachia, na soto tukasimama. Hawa akakimbilia dirishani kwake na kuchungulia nje.
“Kuna nini kinacho endelea?”
“Nahisi kuna uvamizi”
Moja kwa moja nikatambua atakuwa David pamoja na kundi la Zero wamekuja kunisaidia katika mpango wa kuvamia ngome hii.
 
“Mkuu tumevamiwa tunatakiwa kukutoa katika nyumba hii”
Mlinzi wa Hawa aliingia chumba pasipo kubisha hodi na kuzungumza maneno hayo huku akiwa amesimama kikakamavu akimtazama Hawa usoni mwake na wala hakuwa na muda wa kuzungumza na mimi wala kunitazama.
“Siwezi kuondoka humu ndani”
“Mkuu geti kuu tumevamiwa na kundi la Zero, wanaendelea kupambana na wanajeshi wetu, kukaa hapa itakuwa ni hatari kwa maisha yako”
“Bite nielewe basi, nimekuambia sihitaji kuondoka hapa, hakikisheni kwamba ulinzi nje unakuwa mzuri, na waambie kikosi changu chote kwamba wajiweke mbali na hiyo vita na wanatakiwa kuja kuzunguka nyumba sawa”
“Sawa mkuu”
Mlinzi wa Hawa akatoka na kutuacha tukiwa tunasikilizia milio ya risasi jinsi inavyo rindika huko nje.
“Kwa nini hutaki kutoka humu ndani?”   
“Nipo na wewe naamini kwamba kila jambo linakwenda vizuri”
 
“Hawa nisikilize u…..”
“Dany sihitaji kwenda mbali na wewe, pia si yupo Yudia na baba, wataongoza jeshi na watahakikisha kwamba wanawazuia hao watu wa Zero kwa maana ni kundi dogo sana”
Nikamtazama Hawa usoni mwake, nikasikilizia nje jinsi milio ya risasi inavyo zidi kuendelea kusikika. Nikataka kumbuambia Hawa kwamba watu wa Zero wamekuja kunisaidia mimi ila nikashindwa kuzungumza hivyo kwa maana hadi sasa hivi sijajua akili yake inafikiria nini kwenye mpango ambao upo kati yetu kwa maana swala la kumuangamiza baba yake limekuwa gumu sana kwa upande wake. 
“Dany”
“Mmmmm”
“Ninakupenda sana, niliamua kwenda kinyume na baba yangu kwa kukutafuta wewe kwa kupindi kirefu kwa ajili ya upendo wangu kwako. Natambua ya kwamba baba yangu ni mkosaji mkubwa sana kwenye maisha yako ila ninakuomba uweze kumsamehe”
Kabla sijazungumza kitu chochote mlango ukafunguliwa, akaingia mlinzi wa Hawa aliye toka muda machache ulio pita.
“Mkuu nina habari nzuri”
“Habari gani?”
“Watu wa Zero wameweza kudhibitiwa, huku Ziro na Stive wamekamatwa”
“Stive, Stive gani?”
“Yule aliyekuwa mshauri wa Yudia na injinia wa mabomu ya nyuklia”
 
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio baada ya kusikia kwamba Stive amekamatwa.
“Imekuwaje amekuwa msaliti?”
“Bado sijagundua mkuu, labda nifanye uchunguzi”
“Sawa hakikisha kwamba unaniletea habari zote utakazo zifahamu”
“Samahani kwa kuwaingilia”
Mlinzi wa Hawa akanitazama usoni mwangu.
“Unaweza kuniletea taarifa ya wapi atakapo hifadhiwa?”
Mlinzi wa Hawa akamtazama mkuu wake, Hawa akatingisha kichwa kumruhusu kuleta taarifa hiyo ya sehemu ambayo Stive atafungikiwa kisha mlinzi huyu akatoka.
“Walinzi wako una waamini?”
“Yaa hadi kufa kwangu ninawaamini, na wote sidhani kama kuna msaliti kwa maana wamekunywa damu yangu na wameapa kunipigania na kunitunzia siri zangu za ndani hadi dakika ya mwisho ya pumzi zao”
“Wamekunywa damu yako?”
“Ni kiapo ambacho niliwafanyia tangu nikiwa binti mdogo na wengi wao unao waona hapa nimekua nao tangu nilipo kuwa nao watoto”
 
“Sawa”
“Ila huyu Stive sijui ni kwa nini ameamua kumsaliti Yudia na baba kwa maana kinacho kwenda kufwata hapo ni yeye kuuwawa kikatili sana”
“Una muda gani tangu umfahamu Stive”
“Ni mwaka wa nne sasa, kipindi unakuha hapa yeye alikuwa na kazi za nje, na alikwenda kuongoze ujuzi huko Pakistani”
“Ujuzi wa nini?”
“Ujuzi wa kuunda silaha pamoja na mabomu makubwa yakiwemo ya nyuklia”
“Ahaa”
“Ila kwa nini unamuulizia ulizia huyo Stive una mfahamu?”
Nikaka kimya kwa dakika kadhaa huku nikiwa nimetazama chini, taratibu nikakinyanyua kichwa changu na kumtazama Hawa mwenye shauku ya kuhitaji kufahamu jibu la swali lake.
“Yaa nina mfahamu. Stive ni kaka yangu kwa damu moja”
Hawa akashangaa huku macho yakimtoka, ninaamini kwamba hakutarajia kuweza kusikia kwamba mimi na Stive ni mtu na ndugu yake.

AISIIIII……….U KILL ME 117  

“Hahaa, Dany acha kunitania”       
“Niamini mimi, Stive ni kaka yangu”
“Ila mbona hamfanani kabisa”
 
“Undugu sio kufanana ila ni kufaana”
“Hapana Dany kwa hili siwezi kukuami kwa asilimia mia moja”
“Ila kuna ushahidi ambao  yeye anao, unao dhibitisha kwamba mimi na yeye ni mtu na ndugu yake”
“Ushaidi wa kitu gani?”
“Ni video ya marehemu baba yangu”
“Marehemu baba yako!!?”
“Yaaa amenieleza kwamba baba yangu alimuachia video hiyo”
Hawa akaka kimya huku akionekana kutafakari kitu fulani, akapiga hatua hadi kwenye meza iliyomo humu chumbani, akawasha computure iliyopo juu ya meza.
“Unafanyaje?”   
“Huwa kila histori ya mtu kwenye hili ngome huwa inaandikwa na kuhifadhiwa, kwaa ajili ya kutuwezesha kumuamini mtu na kumchukua kiurahisi”
“Unataka kuniambia kwamba nilicho kizungumza kuhusiana na Stive huwezi kukiamini?”
“Yaa asilimia mia moja”
“Mmmm”
 
Hawa akaanza kuminya batani za keyboard ya hii computure, akatafuta jina la Stive, haikuchukua muda sana likaonekena. Taratibu nikayakaza macho yangu kwenye kioo cha computure hii na kunza kusoma historia ya Stive na anaonekena na picha yake pembeni.
“Anaitwa Stivine Kundasemi, uraia wake ni Rwand, amezaliwa mwaka 1983”
Hawa alizungumza huku akinitazama usoni mwangu, sikumjibu kitu chochote zaidi ya kuendelea kusoma historia ya Stive. Stive amezaliwa katika familia ya watoto wanne huku yeye akiwa nimtoto wa tatu, kaka zake walisha uwawa kwenye vita vya Rwanda mwaka 1994”
“Sasa hapo Dany ninashindwa kuelewa unapo niambia kwamba Stive ni kaka yako”
“Una picha zake za nyuma?”
“Ndio hizi hapa”
Hawa akaminya batani kadhaa, akanionyesha picha za Stive tangu alipo kuwa mdogo hadi kufikia ukubwa, kipindi anajiunga na kundi hili la Al-Shabab. Pia nikaona picha za wazazi wa Stive ambao wanafana naye sana uzuri ni kwamba sura zao hazifanani sana na Warwanda.
 
“Tena Stive kabila lake ni Muhutu, na wewe ni Mtanzania halisi, sasa hapa undugu unatokea wapi?”
“Imekuwaje baba yangu ameweza kukiri kwamba Stive ni kaka yangu?”
“Dany kuna mbinu nyingi za mtu kuweza kukiri kwamba nyinyi ni ndugu, na njia ambayo ninaona ilitumika hapo ni kwamba baba yako aliwekewa shinikizo nyuma ya kamera, huwezi jua labda alishikiwa bunduki, au akafanyiwa hila yoyote ya kukufanya kwamba wewe kuweza kumuamini”
Maneno ya Hawa yakazidi kuniingia akilini mwangu na kujikuta nikijilaumu kwa nini ninakuwa na kichwa chepesi ambacho kinanifanya kumuamini kila mtu kirahisi.
“Sijui ni kwa nini Stive alinisaidia”
“Alikusaidia wapi?”
“Nilipo kuwa nimekamatwa na Yudia mapangoni, Stive ndio mtu aliye nitorosha kwa njia za panya hadi tukatokea nchini Kenya”
“Stive ni mpelelezi mzuri sana, alifanya hivyo ninaamini kutakuwa na mbinu ambayo ipo nyumba ya msaada wake, labda bado anafanya kazi chini ya Yudia, na ili kuweza kukupambaza akaona amtumie Stive ili kukupata wewe kirahisi”
“Ninaweza kuipata histori ya baba yangu?”
“Ninaweza kuitafuta kwenye mitandao mingine”
Nikamtajia Hawa jila la baba yangu na kunza kulitafuta.
“Jina la baba yako sio ngeni sana masikioni mwangu”
“Uliwahi kulisikia wapi?”
“Kuna siku nilisikia baba akilizungumza akiwa na K2 kabla hajawa raisi”
 
“Ulisikia wakizungumzia kuhusiana na nini?”
“Kusema kweli sikuweza kufwatilia sana kwa maana mimi na K2 picha haziendi kabisa. Yap nimeipata”
Hawa alizungumza huku akinionyesha histori ya baba yangu, sote tukajikuta tukiwa kimya baada ya kuona picha za mauji ya kutisha ya baba yangu. Japo ninatambua kwamba baba yangu amefariki ila kusema kweli sikuweza kujua amefariki kwa kitu gani. Picha hizi zinaonyesha baba yangu alikufa kwa mateso makubwa sana huko nchini Japan. Baba alimwagikwa tindikali mwilini mwake, kisha akachomwa moto. Sura ya baba ikaanza kunijia kichwani mwangu, nikaanza kukumbuka ucheshi wake na ukarimu alio nionyesha kwangu. Machozi yakaanza kunitiririka taratibu usoni mwangu. Mlango ukafunguliwa kwa haraka nikajikuta nikijifuta machozi na kumtazama mtu aliye ingia humu ndani.
“Mkuu kuna upepelezi unao fanyika kwa kila nyumba humu ndani ya kambi”
“Upelelezi wa nini?”
“Wanamtafuta Dany”
Tukatazama na Hawa sote tukionekana kushangaa.
“Nani aliye sema kwamba Dany yumo humu ndani?”
“Ni Stive, amepewa ruhusa ya kufanya hivyo na Yudia”
“Stive si ulisema amekamatwa na kupelekwa kwenye chumba cha mateso?”
“Stive sio msaliti, amefanya hivyo kwa kutumwa”
“Dany unaona, nilikuambia. Sasa hakikisha kwamba hakuna mpelelezi anaye ingia nyumbani kwangu”
“Sawa mkuu”
Binti huyu akatoka na kunifanya nikae kitandani taratibu huku nikiwa na mawazo mengi kichwani mwangu.
“Walisha kuingiza kwenye mtego Dany, na wakikushika nina uhakika watakua kikatili sana”
Hasira dhidi ya Stive ikaanza kunipanda, nikatamani hata kutoka nje na kwenda kumkamua kwa kadri nitakavyo weza ila nikajikuta nikishindwa kabisa kutokana hata nguvu za mwili wangu zimenipungua tangu niweze kuiona picha ya baba akiwa ameuwawa kikatili.
“Dany, Dany”
“Mmmm”
 
“Nitahitaji nikufiche kwenye chumba changu cha ardhini”
“Kuna chumba cha ardhini?”
“Yaa”
Hawa akatembea hadi kwenye kabati lake la nguo, akafungua milango miwaili ya kabati hili kisha akasogeza nguo, nikaona mlango mwengine ulipo nyuma ya kabati hili lililo jengewa ukutani. Sote tukaingia, na kushuka chini ya ardhi, akawasha taa.
“Kuna kitanda, Tv, bafu na choo vipo hapa. Utakaa huku chini na nitakuwa ninakupa habari kwa kila kitu ambacho kitakuwa kinaendelea huko nje”
“Sawa”
Hawa akanisogelea na kunibusu mdomoni mwangu, kisha akapandisha ngazi kwa haraka, akafunga mlango wa kuingilia ndani ya hichi chumba na kuniacha nikitazama mazingira ya hichi chumba. Nikajilaza kitandani huku nikiwa nimetawaliwa na mawazo na kujiuliza imekuwaje hadi Stive aamue kunidanganya kwamba mimi ni ndugu yake, na hata kama walimshinikiza baba yangu kuweza kukiri kwamba Stive ni kaka yangu, inaonekana kuna mtandao mkubwa sana ambao uliuiangamiza famili yangu, na mtandao huo unasimamiwa na watu wengi wenye nguvu ya kipesa hadi majeshi.
 
“Pesa yangu ingekuwepo, ningeweza kufanikisha kila hambo”
Nilizungumza huku nikiitazama Tv kubwa iliyomo humu ndani ya hichi chumba.
“Siwezi kuliacha jasho la Cajoli limwagike kirahisi namna hii, lazima pesa iweze kurudi”
Nikajilaza kitandani, wala sikuweza kupata usingizi kabisa, masaa yakazidi kwenda kasi. Sikuweza kufahamu ni saa ngapi kutokana sina saa yoyote. Mlango ukafunguliwa kwa haraka nikanyanyuka kitandani huku nikiwa nimeishika bunduki yangu. Nikamuona Hawa akishuka kwenye ngazi huku mkononi mwake akiwa ameshika sahani pamoja na chupa ya chai, ikanibidi kuishusha bunduki yangu chini.
“Habari yako Dany”   
“Salama”
Hawa akaviweka vitu alivyo vishika mezani kisha akanikumbatia, mikono yangu nikipitisha kiunoni mwake, taratibu tukaikutanisha midomo yetu na kunza kunyonyana. Hisia za mapenzi zikazidi kutawala miili yetu, taratibu tukajikuta tukianza kuvuana nguo moja baada ya nyingine. Tukabakiwa na nguo za ndani nikataka kumvua Hawa chupi yake ila akakataa na kuniachia huku akisimama mita chache kutoka sehemu nilipo simama.
 
“Vipi?”   
“Dany siwezi kufanya hivi”
“Kwa nini?”
Nilimuuliza Hawa huku nikimsogelea, akaanza kurudi nyuma na mwisho akajikuta akifika ukutani na mimi nikawa nimesha mkaribia.
“Dany mimi bado ni bikra na nilisha weka kiapo kwa Mungu, nitafanya hivi kwa mwanaume ambaye atanioa tu”
“Hawa umesha kua, hupaswi kuogopa”
Nilizungumza huku nikiushika mkono wa kulia wa Hawa, nikamshikisha jogoo wangu aliyopo ndani ya bokta, akataka kuutoa mkono wake, ila nikamzua na kuendelea kumshikisha jogoo wangu.
“Tazama jinsi ninavyo umia Hawa, mmmmm kwa nini lakini?”
Nilizungumza kwa sauti ya chini sana na yenye msisimko wa mapenzi, Hawa akabaki kimya huku akiwa ananitazama kwa bumbuazi usoni mwake.
“Da….aa”   
“Shii”
Nilizungumza huku nikianza kuzinyonya lipsi zake, Hawa akaanza kulegae tena, nikambeba na kumpeleka kitandani, nikamlaza taratibu na kuendelea kumnyonya midomo yake. Mlio wa simu ukatufanya sote kusitisha zoezi ambalo tunahitaji kulifanya.
 
“Ngoja nipokee simu”
Nikamtazama Hawa usoni mwake kwa sekunde kadhaa kisha nikamuachia, akashuka chini ya kitanda, akatoa simu yake kwenye mfuko wa suruali ambayo alikuwa ameivaa.
“Ni mlinzi wangu”
Hawa alizungumza kabla hajapokeza, nikatingisha kichwa na kumruhusu aweze kupokea simu yake.
“Haloo”
“Baba…..!!?”
“Ninakuja sasa hivi”
Hawa akakata simu na kuanza kuivaa suruali yake.
“Vipi?”   
“Baba anakuja kunitembela huku inabidi niende”
“Sawa”
“Kwani sasa hivi ni saa ngapi?”
“Saa kumi na mbili asubuhi”
Hawa akamaliza kuvaa nguo zake, kwa haraka akapandisha ngazi na kutoka humu chumbani na kufunga kila kitu na nina amini kwamba atakuwa amerudi chumbani kwake. Nikavaa suruali yangu na kuanza kupandisha ngazi kwa utaratibu hadi mlangoni, nikalitega sikio langu kwenye mlango kusikia kitu kinacho endelea. Sikuweza kusikia kitu chochote, nikaa hapa mlangoni kwa dakika kumi, nilipo ona hakuna jambo linalo endelea nikashuka chini, nikafungua chupa ya chai nikamimina chai kiasi kwenye kikombe kilicho kuwa kimefunikia chupa hii ya chai. 
 
‘Kweli nitaweza kupambana na watu hawa wengi nama hii?’
‘Lazima niweze, sitakiwa kuwa mnyonge, waliniulia wazazi wangu, kwa nini na wao niwaache wakiwa hai’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikinywa chai taratibu taratibu. Mlango ukafunguliwa tena, Hawa akashuka kwa haraka na kunifwata kitandani nilipo kaa.
“Kuna lipi jipya?”
“Baba alikuwa ananiuliza kama nimeweza kuona wewe?”
“Kwa nini akuulize wewe?”
“Nahisi kwamba wamenitilia mashaka kwa maana jana sikumruhusu mtu kuingia chumbani kwangu, kwa hiyo nahisi hapo ndipo walipo zidi kupata mashaka kwamba wewe upo chumbani kwangu”
“Umemuona Stive?”
“Yaa ameongozana na baba kuja hapa”
“Nikuombe kitu?”
“Niombe tu kitu”
“Leo ninaomba nianze kufanya kazi yangu kimya kimya kwa maana siwezi kuendelea kukaa humu ndani ikiwa maadui zangu wanazidi kunitafuta kwa ajili ya kuniangamiza”
“Ila Dany bado sijaweka mambo sawa?”
“Hapana wewe niachie tu hiyo kazi, hii ngome ninaijua vizuri sana, so ninakuomba niweze kushuhulikia matatizo yangu yaliyo nileta hapa”
 
“Sawa mimi sina kipingamizi katika hilo. Je kuna vitu vyovyote ambavyo utavihitaji?”
“Ndio, nitahitaji nguo nyeusi tu, sime, bastola mbili, magazine za kutosha”
“Umepata, kitu kingine je?”
“Labda jaketi la kuzuia risasi”
“Poa, nitakoungezee na saa”
“Nitashukuru sana”
“Mbona huli viazi vyangu, ua hupendi kula viazi vitamu?”
“Hapana, ninakula mbona”
Taratibu tukaanza kula viazi hivi pamoja na chai, huku tukisimuliana mambo mengi ya nyuma. Hawa akaniaga na kuondoka, baada ya masaa sita mbele akarudi akiwa na vitu vyote nilivyo muagiza pamoja na ramani inayo onyesha majengo yote ya humu ndani.
“Dany hii kazi ninakuomba uifanye pasipo mtu yoyote kuweza kugundua chochote, kwa njia hii ninaamini kwamba nitaweza kurudi kwenye madaraka yangu”
 
“Sawa sinto kuangusha, ila kama unataka kurudi kwenye madaraka yako ninakusisitizia hawa watu watatu wanatakiwa kuondoka duniani?”
“Nani na nani?”
“Wa ni Stivie, wapili ni Yudia na wa tatu ni…….”
Nikaka kimya huku nikimtazama Hawa usoni mwake, kwa ishara akaniomba nizungumze.
“Wa tatu ni baba yako, nikiimaliza kazi hiyo watu wote ndani ya hii kambi watakusikiliza wewe na kuifwata amri yako na nilazima niweze kuwaua na vibaraka wao kwa maana tukiwaacha hawa vibaraka wanaweza kuja kukudondosha tena madarakani.”
Hawa taratibu akanisogelea hadi karibu na uso wangu, akanitazama kwa macho makavu yaliyo jaa ukakamavu, akavuta pumzi taratibu kisha akaishusha kwa nguvu na kukifanya kifua chake nione jinsi kinavyo shuka.
“Nakuruhusu kumuua baba yangu, ila nitaomba uwe mume wangu hadi kufa kwangu”
Sikutegemea Hawa anaweza kuzungumza maneno kama haya, jambo lililo nifanya nijawe na furaha na taratibu nikampiga busu la mdomo kumuhakikishia kwamba haya matatizo yakiisha nitakuwa mume wake wa maisha yake yote hadi pale kifo kitakapo tutenganisha.

==>>ITAENDELEA KESHO


from MPEKUZI

Comments