Ahadi ya Rais Magufuli kwa Bibi aliyedhulumiwa kiwanja yatimizwa na Waziri Mabula

 Na Munir Shemweta,  Mara
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula amemkabidhi Bibi Nyasasi Masige  Hati za viwanja viwili vilivyopo eneo la Bunda mkoa wa Mara na kutoa onyo kwa wataalamu wa ardhi kutotoa ushauri potofu kwa viongozi wa serikali  wakati wa utekelezaji wa majukumu ya sekta ya ardhi.


Utoaji wa hati kwa bibi Masige unafuatia bibi huyo kuwasilisha malalamiko kwa mhe Rais John Pombe Magufuli  wakati wa ziara yake katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara kutaka kudhulumiwa viwanja vyake. Hati za viwanja  alivyokabidhiwa bibi Masige ni za viwanja  Na 92 na  93/ Kitalu S/ Nyasula C vilivyopo katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara.

Mabula alikabidhi hati hizo pamoja na hati nyingine 92 kwa wananchi wa Bunda leo akiwa katika ziara ya siku tano katika mkoa wa Mara  kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyatoa katika ziara yake ya februari mwaka huu 2018 katika mkoa wa Mara.

Alisema serikali inategemea wataalamu katika kuendesha shughuli zake na kitendo cha wataalamu kutoa ushauri potofu ikiwemo suala la viwanja vya bibi Masige siyo tu kunawapoteza viongozi katika kutekeleza majukumu yao  bali kunachangia kuwepo migogoro katika sekta ya ardhi.

"haiwezekani kupima viwanja na kuchanganya viwanja vidogo, vikubwa na vya kati na kama mtaalamu ukienda kinyume utachukuliwa hatua kwa kutozingatia taaluma."" Alisema Mabula.

Kauli hiyo ya Mabula inafuatia Kauli ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Lydia Mpilipili kueleza kuwa tatizo la viwanja vya bibi Masige lisingefikia hatua hiyo kama wataalam wa ardhi wangetoa ushauri sahihi kwa viongozi wa wilaya katika kushugulikia mgogoro wa bibi huyo.

Aidha,  Naibu Waziri wa ardhi,  Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitoa rai kwa wananchi wakati akikabidhi hati kupeleka kero zao za migogoro ya ardhi kwa viongozi ili ziweze kushughulikiwa sambamba na kutaka watendaji wa sekta ya ardhi kutekeleza maagizo yanayotolewa na viongozi na kuyafanyia kazi .

Bibi Masige alitoa malalamiko ya kudhulimiwa viwanja vyake kwa mhe Raisi wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli wakati wa ziara yake 05 septemba 2018 wilayani Bunda mkoa wa Mara ambapo mhe Raisi aliagiza kusimamishwa kazi kwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa  Joseph Shewiyo  Kwa kushindwa kusimamia agizo la Waziri wa ardhi William Lukuvi kuhusiana na viwanja vya bibi huyo.

Vile. Vile,  katika kutekeleza agizo la Rais Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  naye alifanya ziara katika wilaya Bunda mkoa wa Mara wa lengo la kushughulikia tatizo la bibi huyo tarehe 18 Septemba 2018.



from MPEKUZI

Comments