Waziri Mkuu Kuwa Mgeni Rasmi mkutanowa Wakuu wa Vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya kutoka nchi 54

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi  katika mkutano wa 28  wa Wakuu wa Vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya kutoka nchi 54 za Afrika ujulikanao kama (28 th HONLEA- Afrika).

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar e salaam Kamishna wa Huduma za Mamlaka kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Vallite Green Mwashusa alisema kuwa Waziri Mkuu Majaliwa anatarajiwa kuwa  mgeni rasmi katika mkutano, huo wa 28  wa Wakuu wa Vyombo vinavyopambana na dawa za kulevya kutoka nchi 54 za Afrika unaojulikana  kama (28 th HONLEA- Afrika).

 Kamishna huyo wa Huduma za Mamlaka alisema kuwa “lengo la mkutano huu ni kubadilishana uzoefu na kupanga mikakati ya pamoja kuhusu udhibiti na mapambano dhidi ya dawa za kulevya katika nchi  hizi 54 za Afrika”

Aliongeza kuwa, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Vitendo vya Uhalifu (UNODC) Kanda ya Afrika   imeipa heshima Serikali ya Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo wa 28.

Mkutano huo ambao unaoratibiwa na Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na Dawa za Kulevya na Vitendo vya Uhalifu (UNODC) unatarajiwa kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere kuanzia Septemba 17 hadi 21 mwaka huu.


from MPEKUZI

Comments