Soudy Brown, Maua Sama Watiwa Mbaroni

Msanii wa muziki Bongo, Maua Sama anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Muimbaji huyo anashikiliwa kwa kile kinachoelezwa ni kuweka video mtandaoni akiimba wimbo wake 'Iokote' huku akikanyaga fedha. Pia Maua Sama anashikiliwa pamoja na Mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown.
 
"Ni kweli tunamshikilia msanii Maua Sama kutokana na uharibifu wa pesa hizi za noti za elfu 10, kwa sasa tupo katika mahojiano na ushahidi ukikamilika tutampandisha Mahakamani. Ni kosa kisheria kuchezea fedha za kitanzania kwa mtu yoyote", amesema Mambosasa.

Iokote ni wimbo mpya wa Maua Sama ambao unafanya vizuri kwa sasa, wimbo huo amemshirikisha Hanstone.


from MPEKUZI

Comments