Serikali yapiga MARUFUKU matangazo ya uzazi wa mpango

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya imeeleza kuwa imesitisha matangazo yote ya uzazi wa mpango kwenye vyombo vya habari kwa muda, ili kupitia upya matangazo hayo na kujiridhisha kama maudhui au ujumbe unaotolewa kwenye matangazo hayo unaendana na makusudio ya serikali.

Hayo yamezungumzwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile katika mahojiano yake maalumu aliyofanya na kituo cha runinga cha ITV Tanzania.

Kwa upande mwingine, Mhe. Ndungulile amesema kuwa huduma za Afya na Elimu ya Uzazi wa mpango itaendelea kutolewa kama kawaida isipokuwa ni matangazo tu ndio hayatasikika kwenye vyombo vya habari.

Mwanzoni mwa mwezi huu Septemba, Rais Magufuli akiwa kwenye ziara yake ya kikazi mjini Meatu Mkoani Simiyu, alikaririwa akipingana na masuala ya uzazi wa mpango na kuwataka Watanzania wazaliane bila uoga.




from MPEKUZI

Comments