Serikali Yaomba Kuifanyia Marekebisho Sheria ya Adhabu ya Makahaba ambayo kwa sasa Faini yake ni 500 tu

Naibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamadi Masauni ameliomba Bunge kufanya marekebisho ya sheria ya  adhabu ya makosa ya biashara  makahaba ambapo aliitaja kama ni miongoni mwa changamoto zinazopelekea biashara ya ukahaba kuzidi kufanyika licha ya jitihada za serikali kuitokomeza.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Pwani Zainabu Matitu ambaye alihoji "kwanini Jeshi la Polisi linawakamata wauzaji wa biashara hiyo bila kuwakamata wanunuzi pamoja na wapangishaji wa biashara ya madanguro, ambapo alipendekeza kubomolewa kwa eneo la uwanja wa fisi badala yake kujengwe miundombinu ya maendeleo ili wahusika wafanye biashara halali"?

Akijibu swali hilo Naibu Waziri Masauni alisema “..kumekua na changamoto mbalimbali nadhani bunge hili ni wakati muafaka  wa kuzitafakari, moja ni changamoto ya sheria, ukiangalia kwenye kanuni ya adhabu namba 176  (E) sura ya 16 adhabu ni faini isiyozidi shilingi 500 au 1000.., hivyo kuna haja kuangalia na kutafakari ili kazi kubwa inayofanywa ya kuwakamata wahusika na biashara ya ukahaba iwe na tija…”

Aidha Massauni alisema kupitia Wizara ya mambo ya ndani itashirikisha wizara nyingine ikiwemo Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi, katiba na sheria pamoja na wizara afya ili kumaliza tatizo la biashara ya Ukahaba nchini.

“…Tumendaa mkakati wa kushirikisha taasisi nyingine za serikali kama vile wizara ya  Tamisemi, wizara ya katiba na sheria na pamoja na ustawi wa jamii ili kupunguza na kumaliza vitendo hivi ambavyo ni kinyume na utamaduni wetu.” alisema Masauni.


from MPEKUZI

Comments