Raila Odinga atuma salamu za rambirambi ajali ya MV Nyerere

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu 100 waliofariki mpaka sasa kutokana na kivuko cha MV.Nyerere kupinduka Ziwa Victoria tarehe 20 Septemba 2018 

Katika ujumbe wake alioutuma katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Odinga ametoa pole kwa Watanzania kufuatia ajali hiyo.

“ Naomboleza pamoja na raia wa Tanzania katika kipindi hiki kigumu. Mungu awape amani na nguvu familia, watoa faraja na Taifa la Tanzania,” amesema.

Kivuko hicho kilizama jana mchana Septemba 20, 2018 na hadi leo  Septemba 21, 2018 maiti za watu 100 zimeopolewa.


from MPEKUZI

Comments