Gari La Mbunge CHADEMA Lashambuliwa Kwa Risasi

Gari la mbunge wa viti maalum (Chadema) mkoa wa Manyara, Anna Gidarya linadaiwa kushambuliwa kwa risasi kwenye matairi.

Mbunge huyo amesema kitendo hicho kimetokea leo Jumapili, tarehe 16 Septemba 2018.

Amesema kuwa tukio hilo limetokea kata ya Majengo wilaya ya Monduli mkoani Arusha akiwa anasimamia uchaguzi wa ubunge wa jimbo hilo unaofanyika leo.


from MPEKUZI

Comments