Ubalozi wa Marekani Tanzania watoa ripoti yao juu uchaguzi wa Marudio Uliofanyika Buyungu na Kata Zingine 79

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umetoa taarifa yao kuhusu uchaguzi wa marudio uliomalizika August 12, katika Kata 79 na Jimbo la Buyungu ambapo Mbunge wake alifariki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika website ya US Embassy Tanzania imeeleza kuwa uchaguzi huo uligubikwa na matukio ya fujo na ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi.

Wametoa mfano kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kushindwa kuwasajili baadhi ya wagombea wa upinzani.

Pia umeguswa na vitisho vilivyotolewa na Jeshi la Polisi kwa Wagombea na wanachama wa vyama vya upinzani ikiwemo pamoja na kukamatwa kwa wagombea na kuzuia mikutano ya kampeni.


from MPEKUZI

Comments