Meneja wa WCB, Sallam SK adai hakuna bifu kati ya Diamond na Alikiba

Moja ya mameneja kutoka kwa WCB, Sallam SK amefunguka kuhusu bifu la Diamond la Alikiba.

Katika mahojiano na The Playlist ya Times Fm amesema wasanii hao hawana bifu na kama lipo kuna watu wametengeneza.

"Actually hamna ugomvi, hivi vitu vilitengenezwa na actually watu waliotengeneza wanajulikana, haina haja ya kuwataja kuwa airtime sana," amesema.

"Kati ya Ali na Diamond hamna bifu hata siku moja, haijawahi kutokea na uongozi wa Ali na wetu tunakutana tunacheka na kuongea," amesema Sallam.


from MPEKUZI

Comments