Kubenea adai Hana Mpango wa Kuhamia CCM, Posti yake instagram yajadiliwa kila kona

Na Magdalena Kashindye
MBUNGE wa Ubungo, Saed Kubenea amesema hana mpango wa kuhamia Chama cha mapinduzi CCM kwa sasa.

Kubenea amekuwa akihusishwa kikihama chama chake  cha CHADEMA  tangu mwaka jana, wimbi la viongozi, wabunge na madiwani wa upinzani kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na kujiunga na CCM.

Juzi aliandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akitetea uamuzi wa viongozi wa upinzani kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM.

Ujumbe huo wa mbunge Saed ulisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kuibua mjadala kutokana na kuhusishwa kwake kwa muda mrefu kujiunga na chama tawala.

"Si wote wanaohama wamenunuliwa, ingawa ni kweli kuwa wapo baadhi ya waliohama wamenunuliwa. Kuna wengine wamehama kutokana na kuwapo migogoro, chuki na ubaguzi katika maeneo waliyokuwapo." ilisomeka hivyo posti ya Kubenea

Alipotafutwa na Gazeti la Nipashe, kutaka  kujua juu ya ujumbe wake  alioposti Kubenea alikiri kuuandika na kueleza kuwa kuhamia CCM kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro, kulimsukuma kuandika ujumbe huo.

"Ujumbe huo ni kweli ni wa kwangu," Kubenea alisema, "niliandika baada ya Julius Mtatiro kutangaza kuhama CUF na kujiunga na CCM.

"Inawezekana hakunuliwa, lakini inawezekana njaa ndiyo imempeleka huko kwa sababu kwanza ukumbuke chama chake kina mgogoro mkubwa, pia upande aliokuwa yeye, hakuna ruzuku. Kwa hiyo, hawakuwa na pesa ya kujiendesha na ndiyo maana akaona ahame tu.

"Nasema hivyo kwa sababu kuna baadhi ya watu ambao mimi nawafahamu, walihama na hawakununuliwa isipokuwa walishindwa kuvumilia baada ya kukutana na watu ambao walitofautiana nao kimawazo, yaani mawazo yao yalikinzana, wao badala ya kuvumilia walishindwa."

Alipoulizwa kuhamia CCM  kama naye ni miongoni mwa wanaodaiwa wako kwenye njiani  kujiunga na CCM, Kubenea alisema hana mpango wa kukihama chama chake kwa sasa.

Hii ni mara ya pili kwa Kubenea kukana taarifa za kukihana chama chake kwani wiki chache zilizopita alisema hawezi kahama na kama kunamapungufu watayarekebisha ndani na akishindwa ataendelea na shughuli zake za uandishi wa Habari.


from MPEKUZI

Comments